KOREA KASKAZINI YAIBUKA TENA NA KUFANYA JARIBIO JINGINE LA KOMBORA LA MASAFA MAREFU
Korea
Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora ikiwa ni siku chache tu, tangu
Rais wa Korea Kusini kusema yupo tayari kwa mazungumzo.
Kumekuwa
na shutma kubwa kote duniani dhidi ya hatua ya hiyo ya Korea Kaskazini,
kufanyia majaribio yake zana za nuklia
Marekani
inataka vikwazo zaidi viongezewe taifa hilo huku Ikulu ya White House ikisema
kuwa, Pyongyang imeachwa kutekeleza upumbavu kwa muda mrefu.
Rais
mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in, amelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini,
cha kufanya majaribio zaidi ya zana zake za mafasa marefu, akilitaja kama
kitendo cha uchochezi.
Jeshi
la Marekani limetihibtisha kuwa kombora hilo la masafa marefu, lilirushwa
karibu na mji wa kaskazini magharibi wa Kusong na kuanguka katika bahari ya
Japan.
Moon
ambaye alisema anataka ushirikiano zaidi na utawala wa Pyongyang, wakati wa
kampeni yake, amejibu hatua hiyo kwa kuitisha mkutano wa dharura na washauri
wake wa kiusalama.
Jaribio
lingine la Korea Kaskazini la kuifanyia majaribio zana hizo, liligonga mwamba
wiki mbili zilizopita.
Korea
Kaskazini imekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa pamoja na vikwazo na kufanya
majaribio matano ya zana zake za masafa marefu za nuklia.
Chanzo:
BBC
No comments