KUFATIA KUIBUKA HOJA BUNGENI KUHUSU MSANII DIAMOND KUDAIWA KODI YA MILIONI 400, TRA YATOA UFAFANUZI.
Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha
kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond
Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.
Hayo
ameyasema jana Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa
habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya
ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), jijini Dar es Salaam.
“Tuko
kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi anayopaswa kulipa
Diamond, na kwa bahati nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio
kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza
“Tunajaribu
kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa
kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna
Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo
iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo.
“Hivyo
mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje
ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema.
Awali
akifungua semina hiyo, Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo
kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha
umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa
wananchi.
“Najua
kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu
kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha
serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo
waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma
umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo.
Bwana
Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chombo chenye mamlaka ya
kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi
za umma.
“Huduma
za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi
watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii
waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi
ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.
No comments