SHEIKH JALALA ATOA POLE, KWA WAZAZI NA WAFIWA WA WATOTO WA WANAFUNZI WA SHULE LUCKY VICENT ARUSHA,
Kiongozi
mkuu wa waislam wa dhehebu la washia Tanzania shekh Hemed Jalala ametoa pole
kwa wafiwa wote wa ajali iliyotokea Karatu na kusababisha vifo vya
wanafunzi 32 na walimu wa shule ya
st.Luckys iliyopo mkoani Arusha.
Akizungumza mapema
leo jijini Dar es salaam Shekh Jalala alisema
waislam wa dhehebu la washia wamesikitishwa na kushtushwa na msiba huo
na wanaungana na waislam wenzao ,wakristo pamoja na watanzania wote kwa msiba mkubwa
uliowakumba watoto hao wanafunzi.
Aidha
ametoa pole kwa wazazi na walezi wa
watoto hao na Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Mh.Dk.John Pombe Magufuli
kwa msiba mkubwa ulioikumba taifa letu.
Ajali
hiyo imetokea mkoani Arusha
wilayani karatu na kuua idadi ya
wanafunzi 32 na walimu wawili na dereva
wa shule ya st.lucky.
No comments