SAKATA LA KATIBU MKUU WA CCM MHE KINANA LAIBUKA BUNGENI.BAADA YA MHE LEMA KULIANZISHA AKIDAI AMEFICHWA
Kauli
aliyoitoa bungeni juzi usiku mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema
kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amefichwa ilisababisha mawaziri
wawili wa sasa na mmoja wa zamani wamkomalie kuifuta.
Bunge
lilikuwa likijadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Awali,
Lema alisema ameona kwenye mitandao juu ya Kinana kufichwa na kupaza sauti
akitaka kumtetea akiwa kama Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.
Hata
hivyo, kauli hiyo ilimsimamisha Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene
akitumia kanuni ya 64 (2) ambayo alisema inatoa nafasi kukumbusha Bunge kwamba
kuna kanuni inayovunjwa.
“Mbunge
anayezungumza anasema jambo ambalo hana uhakika nalo, linatia mashaka, sidhani
kama ana uhakika kwamba Kinana amefichwa. Alithibitishie Bunge hili na kama
hawezi kuthibitisha, kupitia kanuni ya 72 (2) nakuomba Mwenyekiti umtake afute
maneno hayo,” alisema Simbachawene.
Ufafanuzi
huo ulimuinua kitini Tundu Lissu na kusema Simbachawene hajui atendalo, Mungu
amsamehe.
“Kanuni
ya 72 (2) inasema mbunge atakayekiuka utaratibu uliowekwa na kanuni hizi
anaweza kutakiwa na Spika hapohapo afuate utaratibu au mbunge atasimama kwa
kutumia utaratibu huo na kutaja kanuni iliyokiukwa,” alisema Lissu.
Baada
ya maelezo hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama ambaye
ni mnadhimu mkuu wa Serikali aliweka msisitizo kwenye kanuni ya 64 (1) (a)
ambayo inakataza mbunge kutotoa taarifa ambazo hazina ukweli.
“Naomba
nimthibitishie mheshimiwa Lema kwamba Kinana tumezungumza naye wakati wa
maadhimisho ya Muungano, wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi. Kinana ametoka
kwenye matibabu na sasa anapumzika nyumbani kwake.
Alipomaliza
kuzungumza Jenister aliinuka Mbunge wa Newala (CCM), George Mkuchika ambaye
aliwahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Nne na
kuomba mwongozo wa mwenyekiti kuwa tangu Lema aanze kuchangia hakuwa
anazungumzia jambo lililoko mezani, yaani bajeti ya wizara ya habari.
“Mheshimiwa
Lema tangu ameanza hakuzungumza habari zozote kuhusu wizara. Mimi kwa umri huu
hata ukinizomea siachi kuzungumza. Mheshimiwa Mwenyekiti naomba muongozo wako
kuhusu kanuni ya 64 (b) inayosema mbunge hatazungumzia jambo nje ya mjadala.
Akitoa
mwongozo wake Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu alisema kwa mujibu wa kanuni
hizi 68 (10) Spika ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu masuala yote ya kanuni,
kwa hiyo akamtaka Lema afute maneno hayo na Lema aliyafuta akisema anafanya
hivyo kwa kuwa waziri amemhakikisha kwamba Kinana hajatekwa.
No comments