RAIS MAGUFULI ATEMBELEA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TAIFA - TBC
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara
ya kushtukiza katika makao makuu ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)
yaliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa mtoa taarifa ambaye hakutaka jina lake kutajwa alieleza kuwa, Rais
Magufuli aliwasili kituoni hapo majira ya saa 5 asubuhi, na miongoni mwa mambo
aliyoyafanya ni kusikiliza changamoto zinazowakumba wafanyakazi wa shirika
hilo.
“Rais
alitembelea hapa majira ya asubuhi na alizungumza na wafanyakazi wa TBC. Ujio
wake ulikuwa ni kwa lengo la kujua hasa changamoto tunazokabiliana nazo katika
eneo letu la kazi,” kilisema chanzo hicho.
No comments