MAAJABU: MTI WAGOMA KUNG'OLEWA KILA UKIKATWA UNALIA KWA SAUTI KUPINGA KUNG'OLEWA MWANZA
Wakazi
wa Barabara ya Iloganzala Jijini Mwanza
jana walipigwa butwaa baada ya mti kutoa sauti kama binadamu ukipinga
using'olewe.
Tukio
hilo limetafsiriwa kuwa la kishirikina ama mazingaombwe ikizingatiwa kwamba si
jambo lenye uhalisia mti kuongea kama binadamu.
Katika
eneo la Iloganzala Jijini Mwanza kuna upanuzi wa barabara inayoelekea Uwanja wa
ndege wa Mwanza.
Shughuli
ya kuung'oa mti huo aina ya mwembe leo
imeendelea ikiwa ni siku ya pili ya kukabiliana na mwembe huo na hatimaye
wamefanikiwa kuung'oa huku mamia ya wananchi wakishuhudia tukio hilo la ajabu
No comments