MHE LOWASSA AMESEMA HAYA MARA BAADA YA KONGAMANO LA DEMOKRASIA KUZUIWA
Mjumbe
wa kamati kuu ya Chadema na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa amelaani
vikali kitendo cha serikali ya Mkoa wa Dar es salam kuzuia kongamano la
demokrasia lililopangwa kufanyika siku ya jana may 13, Mnazi mmoja jijini Dar
es salaam.
Mhe.
Lowassa jana akizungumza na wanahabari
ofisini kwake Mikocheni, Dar alisema kuwa amesikitishwa sana na serikali kuzuia
kongamano ambalo lilikuwa na nia njema ya kuzungumza kuhusu demokrasia na
kujifunza kutoka kwa watu mbali mbali jinsi ya kufanya siasa bila kukosea na
kurekebishana penye makosa.
Mjumbe
huyo aliendelea kufafanua kwamba hakuna tatizo kwa vyama vya siasa kutofautiana
mawazo kwani ndiyo demokrasia na ndiyo sababu kubwa ya waandaji kushirikisha watu wenye taaluma
tofauti tofauti katika kongamano hilo.
"Chadema
kwa ujumla tunalaani sana kitendo cha Serikali ya Dar es salaam kuzuia mkutano
wa amani wa kuwaunganisha watanzania pamoja kwa kutumia kongamano la
demokrasia.
"Kitendo
ambacho kimefanywa ni kuminya
demokrasia. Nia ilikuwa njema na ndio maana waandaji wa kongamano waliweka
picha yangu na kinana tukiwa tunatabasamu hivyo hakuna dhambi kwenye
kutofautiana mawazo"- alisema Lowassa.
Taarifa
iliyotolewa jana kuhusu kongamano.
Hata
hivyo Mhe. Lowassa amekitaka chama cha Mapinduzi kutonyayasa upinzani kwa kuwa
hawataweza kukaa madarakani muda wote huku akiwatahadharisha wakumbuke vyama
vya ukombozi wa Afrika vilivyobaki madarakani ni ANC na CCM.
No comments