MHE GODBLESS LEMA : NYALANDU MUNGU ATAKULIPA
Mbunge
wa Arusha Mjini Mh. Goodbless Lema amemshukuru Mbunge Lazaro Nyalandu kwa
kufanikisha safari ya Marekani ya watoto watatu ambao walinusurika kifo katika
ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent iliyotokea Karatu na kusababisha vifo
vya watu 35.
Mh.
Nyalandu alikuwa bega kwa bega na kufuatilia kila hatua kuhakikisha watoto hao
pamoja na wazazi wao na daktari wanasafiri kwenda nchini Marekani kwa ajili ya
kupata matibabu zaidi.
"Mh
Lazaro Nyalando , Mungu akubariki sana kwa kazi nzuri ya kusaidia watoto
waliopatwa na ajali hapa Arusha, jitihada zako Mungu atakulipa" alisema
Godbless Lema
Katika
hatua nyingine Mh Lazalo Nyalandu ameomba pesa zitakazo endelea kuchangwa na
Watanzania na watu wengine duniani kwa ajili ya watoto hao zitumike kujenga ICU
katika hospitali ya Mount Meru.
"Kwa
kuwa wadau wanaendelea kuchangia na kwa kuwa shule ya sekondari zimekubali
kuanzisha mfuko ambao wanausimamia wenyewe na kwa kuwa mfuko huo lengo lao
kubwa lilikuwa kuwasafirisha hawa watoto kazi ambayo imefanywa na Samaritan
Purse lakini lengo la pili ilikuwa ni kwenda kuwatibu kazi ambayo inafanywa na
Shirika la STEMM kwa kushirikiana na Hospitali kuu ya Mercy.
hivyo
kazi itakayobaki Mh Mkuu wa Mkoa itakuwa ndogo, kwa hiyo nimeomba na
nimeshaurina nao na wamekubali kwamba Watanzania na wanadunia wote watakao
endelea kuchanga fedha zote ziletwe kwako Mh Mkuu wa mkoa ili ziweze kujenga
kituo cha wagonjwa ambao wanahitaji huduma ya haraka (ICU) katika hospitali
yetu ya Mount Meru" alisema Nyalandu
No comments