HII NDIO KAULI YA MHE SALMA KIKWETE ALIYOWAGAWA WABUNGE BUNGENI
Mchango
wa Mbunge wa Kuteuliwa(CCM), Salma Kikwete kuhusu kupinga wanafunzi wanaopata
mimba wakiwa shuleni kuruhusiwa kuendelea na masomo jana ulizua gumzo bungeni
kutokana na wabunge kugawanywa na suala hilo.
Hali
hiyo ilijitokeza wakati wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa Fedha 2017/18 bungeni jana.
Salma
amesema anapinga suala la watoto wanaopata ujauzito shuleni kuendelea na masomo
kutokana na mila, desturi, dini na mazingira.
Ameitaka
Serikali kutafuta njia nyingine ya watoto hao kupata elimu badala ya kuwaruhusu
kuendelea na masomo.
Akitoa
taarifa yake kwa mchangiaji Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy
alitaka mbunge yeyote ndani ya Bunge ambaye alianza kushiriki mapenzi akiwa
shuleni atoe ushuhuda bungeni kama aliweza kuendelea vizuri kimasomo.
Amesema
anaunga mkono wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni wasiruhusiwe kuendelea
na masomo
No comments