KUFATIA KUSAMBAA ORODHA YA MAJINA YA POLISI WENYE VYETI FAKE, JESHI LA POLISI LATOLEA UFAFANUZI.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi5QIgrEgSOYFISl2A0kM4u-2tJ8dENx1yFTBauu0co6ofcBB7-nqplblycXLkrgmwUWEgvUpALZkoO7-cXOvEOV8RSRDv03EUPRiOBU96nBNCFm-u8NU_FtKm3_bJe68BQphFCSxFn9vFa/s640/1.jpg)
Jeshi
la Polisi nchini limekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii
zikiwahusisha askari wake kuwepo katika majina ya vyeti feki na kusema taarifa
hizo ni za uongo na wala hazijatolewa na Jeshi hilo.
Hayo
yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, ACP Advera
Bulimba na kusema wanaendelea kumtafuta mtu aliyesambaza taarifa hiyo kwa lengo
la kupotosha umma ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake na kuwa
fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
"Jeshi
la Polisi nchini, linaujulisha umma kwamba, orodha ya majina ambayo yamekuwa
yakisambazwa kwenye mitandao ya kijamii yakidai kuwa ni majina ya askari wa
jeshi la polisi wenye vyeti feki ni ya uongo na wala taarifa hiyo haijatolewa
na jeshi la polisi". Ilisema taarifa hiyo
No comments