Awali
waraka huu ulisambaa kwa kasi ya ajabu mtandaoni
WARAKA
YA WAZI KWA UONGOZI WA SAHARA MEDIA GROUP KUHUSU KIPINDI CHA TUONGEE ASUBUHI
KINACHOTARAJIA KURUSHWA JUMATATU YA TAREHE 22/5/2017
Anaandika
William Bundala
(Kijukuu
Cha Bibi K)
Habari
ya wakati huu uongozi wa Kampuni ya Sahara Media hususan wahariri wa Star Tv Mwanza na Dar es salaam,Mimi ni
mzima wa Afya tele licha ya hali ngumu ya maisha tuliyonayo kwa kipindi hiki
cha mpito.
Mimi
naitwa William Bundala jina maarufu Kijukuu Cha bibi K,Ni mtangazaji wa na
Mwaandaaji wa Vipindi Radio Free Africa,Nimeamua kutumia nafasi hii kuwaandikia
viongozi wangu wa Sahara hususan ni Star Tv.
Ndugu
zangu siku za hivi karibuni nimeona kipererushi mitandaoni kikionyesha kuwa
Kituo chetu cha Star Tv kitarusha mahojiano ya Mkuu wa mkoa Fulani katika
kipindi cha TUONGEE ASUBUHI,Nianze kwa kuwapongeza upande wa jinsi
mlivyotengeneza kipeperushi (Cover) na kukisambaza katika mitandao ya kijamii.
Nimeona
jitihada za usambazaji katika Magroup ya Whattupp,Instagram,Facebook,Twitter na
maeneo mengine mengi,Hakika Tanzania na nje ya Tanzania asilimia kubwa watu
wameona mwaliko huu ambao kwa upande wangu mimi sijaona umuhimu wake hata
chembe.
Ndugu
zangu Star Tv ukweli usiyofichika ni kwamba siku ya kurusha kipindi hiki
tutatazamwa sanaa na idadi kubwa ya watu ila idadi hiyo ya watu itakayotutazama
ndiyo itakuwa mabalozi wa kuwaondoa wengine wasitazame Tena Star Tv labda
watasalia wachache ambao naamini kusalia kwao ni kutokana na Kipindi cha FUTUHI
tu.
Ninachoandika
hapa naomba kwanza ieleweke ni utashi wangu binafsi na hakuna mtu aliyenisukuma
katika hili,na andiko hili lisihusishwe na maswala yoyote ya kisiasa,kidini
wala kikabila bali ni katika kujengana na kufanikiwa kuinua kituo chetu.
Ieleweke
kuwa kwa sasa tunatakiwa kufanya vitu vingi vya kijamii ili kuwarudisha
watazamaji wetu kuwa na imani na chombo chetu,Nasema hivi nikikumbuka namna
tulivyokuwa tunasemwa vibaya wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.
Tumesemwa
sanaaa kwenye mitandao ya kijamii lakini zaidi hata sisi tunaopenda kukaa
kwenye Stuli ndefu tulikuwa hatuna furaha kutokana na kusemwa sanaa kuhusu
kampeni za uchaguzi huo.
Tungali
bado tunamalizia kuuguza makovu ya kusemwa vibaya tangu uchaguzi wa mwaka 2015 naona kila dalili za kidonda cha
kusemwa vibaya kurudi tena mara ya pili hii ni baada ya kwenda hewani kwa
kipindi hiki ambacho nimeona katika kipeperushi kipya kuwa kitakuwa ni
jumatatu.
Ninazo
hoja chache za mimi kupinga kipindi hiki kwenda hewani,Siwezi kuzuia kisiende
kutokana na nafasi yangu bali naweza kushauri na mkaangalia upya mfanye nini
jumatatu kuliko kuruhusu kipindi hicho kwenda hewani.
Ngudu
yangu Kaka yangu mshauri wangu wa maswala ya Media Paul Mabuga najua sanaa
uwezo wako katika Tasnia ya habari je hili swala mmelichuja na kuona faida na
hasara zake kwa Chombo chetu cha Star Tv?
Kaka
yangu rafiki yangu Moses Buhilya Program Manager Star Tv kama sijakosea cheo,Je
umekaa chini na waandaaji wa hayo mahojiano kujua nini wanahitaji kumuhoji mkuu
huyo wa mkoa?
Sitaki
kuongea chochote kwa wapiga picha ambao watashika camera siku hiyo kwani katika
hili sijaona kama wana madhara katika kutekeleza majukumu yao.
Ninayo
mambo machache ya kuhoji na kushauri kuhusu kipindi hiki:-
(1)Naomba
kurudia tena kuwa tutafanikiwa sanaaa kutazamwa na watanzania wengi na hata
wasiyo watanzania kutokana na mambo lukuki ambayo watanzania wanataka kuyajua
kutoka kwa mgeni atayehojiwa siku hiyo,Lakini katika hili naomba kuwaambia kuwa
baada ya kipindi kuisha watazamaji hao watakimbia,Ni vigumu kujua watakimbiaje
maana hatuwezi kujua kama watatazama au laa.
(2)Mtu
anayehojiwa namfahamu vizuri katika zana nzima ya kuongea anaweza sanaa kuongea
na anaijua Media vilivyo,Hofu yangu inakuja hao watu ambao mmewateuwa kufanya
naye mahojiano,Hofu hii inakuja kutokana na ukweli kuwa Mgeni atabadilika kuwa
mwendesha kipindi na waandesha kipindi kugeuka kujibu maswali na kuitingisha
kichwa kukubali atakachokisema mgeni kutokana na uwezo wake alionao.Sibezi kama
watakaohoji hawajui HAPANA bali kama mtafanya akikisheni IQ ya watangazaji iwe
kubwa sanaa katika kuhoji na kuuliza maswali kuliko IQ ya Mgeni.
(3)Jambo
la tatu ambalo ndiyo kubwa katika waraka huu ni kutaka kujua kama Jukwaa la
wahariri Tanzania (TEF) tayari wameruhusu Huyu mgeni anayetaka kohojiwa
jumatatu ahojiwe,maana nakumbuka walitoa tamko hakuna chombo kinachoruhusiwa
kutoa habari zake,Niwakumbushe tu kuwa agizo hilo la baraza la wahariri
Tanzania (TEF) kwa kushirikiana na Klabu ya waandishi wa habari Dar es saalam
(DCPC) lililoungwa mkono na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania
(UTPC) lilitolewa Tarehe 22/3/2017.
Katika
Agizo hilo walibainisha mambo ambayo waliyohuzinishwa nayo yaliyofanywa na
Mgeni huyo mnayetaka kumwalika na kisha kutoa hatua tatu za kuchukua
Katika
barua hiyo walisema,Tafadhali Soma hapa chini kupitia link ya Mpekuzi
http://www.mpekuzihuru.com/2017/03/tef-yamtangaza-makonda-adui-wa-uhuru-wa.html
Bada
ya kusoma link hiyo tujiulize kabla jumatatu haijafika je Waliotoa agizo hilo
wamesharuhusu kufanya naye vipindi? Na kama bado hawajaruhusu je sisi Star Tv
agizo hilo halituhusu na kama linatuhusu je wapi tunapata nguvu ya kwenda
kinyume na Agizo la baraza la wahariri Tanzania?
(4)Tangu
niajiriwe hapa Sahara Media tangu Mwezi wa 10 mwaka 2013 sikuwahi kuona
mahojiano ya mgeni huyu anayetarijiwa kufanya nasi kipindi maalumu cha Toungee
Asubuhi siku ya jumatatu,Nimezoe kuona taarifa za habari tu ambazo zinaandikwa
na waandishi wetu wa Dar es salaam lakini vipindi vya namna hii nimeona katika
Tv zingine za Dar es salaam na siyo hapa kwetu,Je nini kimetokea mpaka
mahojiano haya yafanyike hapa kwetu?..Nakumbuka sisi Radio free Tuliwahi
kumpigia simu tukihitaji kufanya naye mahojiano kuhusu kauli yake ya kutaka
Benki impe maelezo kuhusu inawezekanaje watunishi hewa kuchukua mishahra
kupitia Bank? lakini hakutupa ushirikiano badala yake alitujibu vibaya kwa
kutwambia sisi hatujui mkuu wa mkoa ana mamlaka gani na kuongeza kuwa ndiyo
mana Hatuendelei.Je leo ametuona Sahara Media na Vyombo vyake tunajua mamlaka
ya mkuu wa mkoa na ndiyo mana ametaka kufanya mahojano na sisi?
(5)Kuna
swala linaandikwa mitandaoni na baadhi ya watu kuwa waandaaji wa kipindi hiki
cha jumatatu wanatafuta Kujijenga wenyewe na siyo kukijenga kituo,Mimi sitaki
kuamini hili ila lisemwalo na mtu mzima usilipuuze,Nashindwa kukataa kwa
asilimia 100 kutokana na promotion ya hii kitu nashawishika kukubali,Kwanza
nina imani Mgeni atakuwa katika ofisi ya Dar es salaam na wengine watakuwa
ofisi za Mwanza,Swali linalokuja kichwani mwangu kwanini kwenye kipeperushi
wawekwe watangazaji wa wa Mwanza ambao hawatakuwepo na Mgeni studio? Je picha
za watu watakaokuwa studio ya Dar es salaam hazipo au hawana umuhimu katika
kipererushi hicho? Kwanini tusiamini kuwa hiki kipindi kinatafuta umaarufu
kumjenga mtu na siyo kituo?
(6)Amini
nawaambia mara baada ya kipindi hiki kurushwa vyombo vyetu vitashambuliwa
sanaaa na kutengwa,Mkuu wangu boss wangu Osolo Nyawanga wewe ni Mwenyekiti wa
Chama cha waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza(MPC) Ambao mpo chini ya Umoja wa
klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Ambao nao wameunga mkono kuwa
hakuna chombo kinachoruhusiwa kutoa habari za mtu huyu,Je Kiongozi wangu Osolo
umelitazama hili kwa jicho la FAIDA na HASARA?
(7)Nduu
zangu viongozi baada ya kipindi hiki kuruka tujiandae kuandikwa kwenye
mitandao ya kijamii na kusemwa kwa
kwenda kinyume na vyombo vingine ikiwa ni pamoja na kuanza kuvuliwa nguo
viongozi,watangazaji na kampuni kwa ujumla,Usije kushangaa yakiandikwa mengi
mpaka kuhusu Kiwango cha elimu cha watu waliondaa mahojiano hayo,Machache
yameanza kusemwa kuwa mmoja kati ya watu watakaongoza kipindi hicho sijui wa
Dar au Mwanza hana cheti badala ya kushindwa kumaliza masomo ya Certificate
katika moja ya chuo cha habari kanda ya ziwa,Kama yameeanza haya kipindi
hakijaruka mnategemea nini kipindi kikiruka? Chonde chonde Viongozi wa Star
Tv……”YA NGOSWE TUMWACHIE NGOSWE”.
(8)Swala
lingine tusiangalie watazamaji wa siku moja ila angalieni je Tv inatakiwa
kuishi miaka mingapi?,Tumesahau kuwa mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi gari
letu la Mahidra lililokuwa likiendeshwa
na dereva Gerlad Swai lilipigwa Mawe eneo la Pasiansi na tukaamua kubandua
Lebel (Vipeperushi ) kwenye magari vinavyoonyesha magari ni ya Kampuni ya
SAHARA MEDIA,Je hili mmelisahau wenzetu?Tafadhali tupime faida tutakayopata
kama chombo Star Tv na hasara yake kwetu kama kampuni kabla ya kuangalia kitu
kimoja tu kuwa tutatazamwa sanaa.
(9)Mimi
sina piamizi na wazo la kurusha kipindi hiki,ila hofu yangu ni hayo ambayo
nimeyaeleza hapo juu,kama kampuni na uongozi wa Star Tv mtakuwa tayari
kupambana na hayo ambayo naamini siyo yote
yatatokea niwatakie kila la kheri na mimi nitakuwa mtu wa kwanza
kuangalia kipindi hicho.Na kama kuna maagizo maalumu kutoka ngazi ya juu ya
Serikali naomba waraka huu upuuzwe kwa nguvu zote lakini kama hakuna maagizo ni
maamuzi tu ya waandaaji wa kipindi cha TUONGE ASUBUHI Nawasihi angalieni upya
swala hili kabla ya jumatatu kufika.
(10)Mwisho
lakini si kwa umuhimu,Naomba nisijadiliwe vibaya na kuonekana nipo kinyume na
kampuni iliyoniajiri,Bali mawazo haya yapokelewe na yafanyiwe kazi kama
yanafaa,Sina chuki na Mgeni,Sina chuki na watangazaji watakaohusika kuendesha
mahojiano wala sina chuki na kampuni yangu,Bali kwa akili zangu nimewaza
nikaona hili swala litatugawa na kuibua mwanzo mpya wa mengi ndani ya kampuni
yetu.
MY
POINT:
“DON’T
PUT YOUR MOUTH ON MOTION, WHILE YOUR BRAIN IS ON GEAR”
Ndimi
William
Bundala
(Kijukuu
Cha Bibi k)
0767-942570
0786-942570
E-mail
bundala.william@yahoo,com
|
No comments