KAULI YA MWENYEKITI WA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA ARUSHA BAADA YA WAANDISHI KUKAMATWA KISHA KUACHIWA WAKIAMBIWA WALIPEWA 'LIFT' TU
Mwenyekiti
wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Claud Gwandu
Leo
Arusha kumetokea tukio la Polisi kuvamia mkusanyiko wa watu walioongozwa na
Meya wa Arusha kwenda kutoa rambirambi kwa familia zilizopata msiba kwenye
ajali ya Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.
Tukio
hilo ambalo pia lilihudhuriwa na Madiwani, Waandishi wa habari na viongozi
mbalimbali wa dini (Wakristo na Waislamu) lilifanyika kwenye eneo la shule hiyo
ya Lucky Vicent ambapo wakati wakiendelea kuzungumza wakiwa gorofani ghafla
waliona Polisi wamefika kwa spidi na kusema watu wote wako chini ya ulinzi.
Baada
ya hapo Polisi waliwakamata na kuondoka nao wote wakiwemo Waandishi wa habari
wapatao kumi ambapo baada ya kufika kituo cha kati cha Polisi, Waandishi hao
waliachiwa huru huku Polisi wakiwaambia hawana shughuli nao bali waliwapa lift
tu kutoka kwenye eneo la tukio.
Kwenye
mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika dakika chache baadae, Polisi
walisema alieamuru Waandishi kuwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kituoni
hakufahamu kwamba hao ni Waandishi na kwamba Wanahabari hao hawana kosa lolote
na ndio maana waliachiwa muda mfupi baada ya kufika kituoni.
Kufuatia
tukio hilo,Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) imelaani tukio
hilo.
"Tulikuwa
tunahangaikia wenzetu waachiwe kwanza na hatimaye tumefanikiwa,wameachiwa huru
bila masharti yoyote....maelezo ya kaimu RPC yanakera na kuchekesha,na kwa
kweli ni kama kejeli....Eti waandishi hawakukamatwa bali walipewa 'lift' na
Polisi kuwarudisha mjini wakati walienda na magari yao na yamebaki shuleni
Lucky Vincent,ni jambo gumu kueleweka",ameeleza mwenyekiti wa klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Claud Gwandu.
"Awali
waliambiwa kuwa wamekamatwa kwa kukutwa kwenye mkusanyiko usio na kibali lakini
waliokamatwa ni waandishi 9, meya wa Arusha,diwani mmoja na viongozi wawili wa
dini..Hivyo basi,uongozi wa APC,pamoja na kulaani unyanyasaji huo wa wazi kwa
.maelezo ya kina kuhusu kukamwaandishi wa habari,utaandika barua ya malalamiko
kwa uongozi wa Polisi Mkoa kutaka atwa kwa wanahabari hao na baada ya hapo
utachukua hatua stahiki",ameongeza Gwandu.
Katika
hatua nyingine meya wa jiji la Arusha,madiwani,walimu,mmiliki wa shule ya lucky
Vincent,viongozi wa dini waachiwa huru kwa dhamana kwa masharti kwamba
watakapoitajika muda wowote wafike.
Inaelezwa
kuwa wamepewa dhamana baada ya polisi kutaka hizo rambirambi zikabidhiwe
kituoni hapo ili ufanyike utaratibu mwingine wa kuwafikishia walengwa jambo
lililopingwa vikali na meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro.
No comments