KADA WA CCM AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIBITI
Katibu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Kata ya Bungu wilayani Kibiti, Alife Mtulia ameuawa kwa
kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema mauaji hayo yamefanyika usiku wa kuamkia
leo (Jumapili) katika Kijiji cha Nyambunda.
Amesema Mtulia
aliuawa na watu hao alipokuwa anakwenda kuoga.Kamanda amesema mwili wa marehemu
umepelekwa kituo cha afya cha Kibiti kwa uchunguzi.
Mauaji ya askari
Polisi, viongozi wa Serikali za Mitaa na raia yamekuwa yakifanyika mara kwa
mara katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.
Jumanne wiki hii
akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba aliliambia Bunge kuwa Serikali itaanzisha mkoa mpya wa kipolisi
katika wilaya za Kibiti, Rufiji, Mkuranga na Mafia. Utaitwa mkoa wa kipolisi
Rufiji.
No comments