DC MJEMA AMWAGIA SIFA RAIS MAGUFULI
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kutoa fursa adhimu ya kukimbiza mwenge wa Uhuru katika wilaya yake
sambamba na kuzindua pamoja na kuhamasisha shughuli mbalimbali za
maendeleo.
Mh.Mjema amesema kuwa kwa kuzingatia hoja na
vipaumbele vya serikali ya awamu ya tano Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2017 umebeba kauli mbiu isemayo “Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa
Maendeleo ya nchi yetu” ambapo katika kutimiza azma hiyo ya serikali ya
manispaa ya Ilala imewewka mikakati shirikishi ya uanzishaji, uendelezaji na
usimamizi wa viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya maendeleo ya 2025.
Mh.
Mjema amesema kuwa halmashauri ya manispaa ya Ilala imetenga zaidi yay a hekta
289 ili kuanzisha maeneo maalum kwaajili ya uwekezaji (EPZ) na kuyataja maeneo hayo kuwa ni Bonde la Msimbazi,Tabata,Luhanga,Kiboga
na Msongola, Bangulo, Mji mpya Majohe, Yongwe, Chanika na Vingunguti sambamba
na kutenga mitaa ya viwanda vidogovidogo kama vile Gerezani
Aidha
Mjema amesema kuwa kwa pamoja wanaunga mkono vita dhidi ya dawa za kulevya pamoja na kuhakikisha vitendo vya rushwa
vinatokomezwa nchini.
Mkuu
wa Ilala Mh.Mjema amebainisha mwenge wa Uhuru unapitia jumla ya miradi tisa ya
maendeleo ambapo shughuli za kuweka mawe ya msingi, kukagua na kuzindua miradi
hiyo yote ina jumla ya thamani ya shilingi zaidi ya Bilioni 14.