WAZIRI MKUU MAJALIWA AMTAKA MKUU WA MKOA WA PWANI KUWASAKA WAFUGAJI WANAODAIWA KUWAPIGA WAKULIMA BAGAMOYO

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo kupiga
kambi katika Kata ya Miono wilayani Bagamoyo na kuwasaka wafugaji wanaopiga
wakulima.
Waziri
mkuu alitoa agizo hilo alipozungumza na wakazi wa kata hiyo hivi karibuni alipokwenda
kukagua miundombinu ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo wilayani Bagamoyo
mkoani Pwani.
Taarifa
ya Ofisi ya Waziri Mkuu ilisema diwani wa Miono, Juma Mpwimbwi akiwasilisha
kero zao kwa kiongozi huyo alisema wanakabiliwa na tatizo la wakulima kupigwa
na wafugaji na wakipelekwa kituo cha polisi hawachukuliwi hatua.
“Wafugaji
wanatupiga lakini wenzetu hawachukuliwi hatua na hata ukienda kushtaki polisi
hawakai kwa sababu wanadai wao wana fedha,” alisema diwani huyo.
Pia,
alisema waliahidiwa barabara ya lami tangu miaka saba iliyopita, lakini hadi
sasa hawana hata kipande kidogo tu cha barabara hiyo.
Mkazi
wa kata hiyo, Shabani Mkwimbi akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake alisema
wana kituo cha polisi na mahakama, lakini utendaji kazi wa viongozi waliopo
unatia shaka.
Alimlalamikia
mkuu wa kituo cha polisi na hakimu akidai wafugaji pekee ndiyo wanaoshinda
kesi.
Waziri
Mkuu Majaliwa aliwahakikishia wakazi hao kwamba hakuna hata mtu mmoja ambaye
yuko juu ya sheria. Alisema suala la polisi litashughulikiwa na kamanda wa
mkoa.
Majaliwa
alisema msimamo wa Serikali ni kuwaona wakulima na wafugaji wanafanya kazi zao
kwa uhuru.
“Hakuna
mfugaji anayeruhusiwa kupeleka ng’ombe kwenye mashamba yenye chakula. Mkuu wa
mkoa hili ni agizo, njoo upige kambi hapa na watu wako, na usake wahusika hadi
wabainike. Ni lazima tuwajue ni kina nani wamehusika na hili,” alisema.
Advertisement
==
Bonyeza
HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari
zetu Haraka
No comments