DKT BILAL JAMII IWAJALI NA KUWASAIDIA WATU WENYE USONJI
Makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya nne mhe Dkt Mohamed Gharub Bilal ametoa wito kwa taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kujitokeza kusaidia watoto wenye ugonjwa wa usonji jambo litakalosaidia kuwafanya watoto hao kujiona ni sehemu ya jamii.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa matembezi siku ya usonji duniani yaliyondaliwa taasisi ya KSIJ Center of education katika shule ya Al Mutazar mapema leo jijini dar es salaam alisema jitihada za pamoja zinatakiwa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakuwa na furaha na amani hivyo kujiona sawa na wengine.
Alisema natoa pongezi hatua iliyochukuliwa na tasisi ya KSIJ Center of education ya kuanzisha kitengo chs maalum kitakachokuwa kinatoa mafunzo kwa watoto wenye usonji ni swala la kuungwa mkono kwani kazi hiyo ina changamoto nyingi ikiwemo fedha , wataalamu pamoja na aslimali watu.
Dkt bilal aliongeza kuwa kwa kutambua athari za ugonjwa huo wa asonji ipo haja kwa jamii kujitoa kwa hali na mali hili kuwafanya na wao kujisikia kuwa ni sehemu ya jamii kwa kuwapatia misaada mbalimbali.
Adiha dkt bilal alisema katika kuhakikisha anaunga mkono juhudizilizoonyeshw na taasisi ya KSIJ Center of education katika kusaidia watu wenye usonji amechangia mil 1.5 na kuongeza kuwa makamu wa rais mhe samia sukuhu hasani atachangia mil 5.
Mapema akizungumza wakati akimkalibisha mgeni rasmi Mwenyejkiti wa Taasisi ya KSIJ Center of education bwana Imtiaz Lalji alitoa wito kwa jamii kuwa karibu na watu wenye ugonjwa wa usonji sambamba na kuwasaidia kuwawezesha kutimiza ndoto zao.
Alisema kupitia taasisi ya KSIJ Center of education tayali wameshatoa mafunzo kwa wanafunzi watatu wenye usonji na mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo wamewaajilikama walimu wasaidizi shuleni hapo hivyo kutoa wito serikali pamoja na taasisi zisizo za kiserikali kuanza kutoa nafasi za ajila kwa watu hao.
Maadhimisho ya siku ya usonji mwaka huu yanaadhimishwa duniani leo na kupewa kaulimbiu isemayo “Tuwalinde na Tuwapende”
No comments