WAKUU WA MIKOA, WILAYA WANUSURIKA SAKATA LA VYETI FEKI
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi Bora Mhe. Angellah Kairuki amebainisha baadhi ya
mambo waliyokuwa wameyapa kiupambele katika zoezi zima la uhakiki wa vyeti feki
kwa kusema zoezi halikuweza kuhusika na viongozi wa kisiasa.
Kairuki amebainisha
hayo leo katika ukumbi wa Chimwaga uliopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma,
wakati anatoa taarifa ya uwasilishaji wa uhakiki wa vyeti feki kwa Watumishi wa
Umma lilioendeshwa na Serikali kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2016.
"Zoezi hili la uhakiki
wa vyeti feki halikuwahusisha viongozi wa kisiasa kama Wabunge, Mawaziri, Wakuu
wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, kwa sababu kwa mamlaka za uteuzi wao wanahitajika
kujua kusoma na kuandika tu...Watumishi 9,932 wamebainika kuwa na vyeti vya
kughushi sawa na asilimia 2.4 . Wenye vyeti vya utata ni 1,538 vilikuwa
vikitumiwa na jumla ya watu 3,076, wenye vyeti halali pekee ni asilimia
94...Hatua hazitachukuliwa kwa wenye vyeti feki tu, bali hata kwa wanaohusika
kutengeneza vyeti hivyo". Alisema Kairuki
Aidha Mhe. Kairuki
amewataka wale wote wanajijua wanatumia vyeti vya kughushi waache mara moja kwa
kuwa ni kosa la jinai huku akisisitiza kuwa adhabu yake ni kufungwa jela miaka
saba.
Pamoja na hayo, Kairuki
amepongeza serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuamua
kushughulika na zoezi hilo na kulimaliza kwa awamu moja tofauti na nchi
nyingine zilichukua awamu tatu huku akitolea mfano wa kwa kuzitaja nchi hizo
kwamba ni South Africa na Nigeria.
Kwa upande
mwingine, Rais Dkt. Magufuli amewaagiza
Waziri Kairuki na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwaondoa watumishi wote
waliobainika kuwa wanatumia vyeti vya kughushi 'hewa' huku akisisitiza kwamba
yeye hawezi kuwasemehe watu walioghushi kwani wataondoka mara moja.
No comments