POLISI KANDA MAALUMU YAPIGA MARUFUKU CUF YA MAALIM KUFANYA USAFI BUGURUNI JUMAPILI
Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imezuia wanachama wa CUF kufanya usafi katika
makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni kutokana na kuwepo kwa viashiria
vya uvunjifu wa amani kutokana mvutano wa makundi mawili.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon
Sirro amesema ombi la kufanya usafi katika mazingira ya ofisi za chama hicho,
liliwasilishwa na Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea Aprili 27 mjini Dodoma.
Amesema
kutokana na sababu za kiusalama pamoja na mgogoro wa muda mrefu unaoendelea
ndani ya chama hicho, Mbunge huyo pamoja na wanachama wengine wanashauriwa kila mmoja kufanya usafi katika
eneo lake analoishi au analofanyia kazi.
"Kitendo
hicho cha wanachama wa CUF kukusanyika kutoka katika maeneo mbalimbali kwa
kigezo cha kufanya usafi kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani na
atakayethubutu kujitokeza atachukuliwa hatua za kisheria," amesema Sirro.
Wakati
huo huo Kamanda Sirro amesema sakata la watu waliovamia mkutano wa iongozi wa
CUF wilaya ya Kinondoni na wanahabari hadi sasa wanawashikilia watu saba
akiwemo Mkurugenzi wa Mahusiano wa wa chama hicho, Abdul Kambaya.
Amesema
upelelezi wa kesi hiyo, umefanyika vizuri na tayari jalada limefikishwa kwa
Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Jeshi
hilo pia limewataka wananchi waliowahi kuibiwa magari yao kujitokeza katika Kituo
cha Polisi Mbezi ili kuangalia kutokana,na kupatikana kwa magari matano
yanayodaiwa kuibiwa jijini Dar es Salaam.
No comments