UPINZANI WAGOMA KUSOMA HOTUBA YAO BUNGENI
Msemaji wa upinzani katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na
Muungano, Ally Salehe amesusa kusoma hotuba yake ya upinzani kuhusu wizara hiyo
baada ya kulazimishwa kuacha kusoma baadhi ya maneno yakiwamo yanayohusu
Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar na mgogoro wa CUF.
Hali hiyo imetokea bungeni leo Jumatatu baada ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), George Masaju kusimama na kupinga baadhi ya
maneneo aliyotumia kama “Kila wizara imekiona cha moto, wamebanwa mpaka
wamevunjwa mbavu” na kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeathirika vibaya na kisu
cha ngariba kwa kukata bajeti yake.
Baada ya malumbano, Mwenyekiti wa Bunge, Musa Zungu alitoa
uamuzi kuwa maneno yaliyoandikwa kuanzia ukurasa wa tatu hadi wa saba kwenye
hotuba hiyo yasisomwe wala kurekodiwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge.
Baada ya uamuzi huo, Salehe alisema basi asingeendea kuisoma
hotuba yake na yaliyobaki anamwachia ngariba afanye anavyotaka
No comments