NAIBU WAZIRI WA AFYA MHE KIGWANGALLA AMMWAGIA SIFA DIAMOND PLATNUMZ
Siku chache baada ya staa mwimbaji Diamond Platnumz kuzindua
Perfume yake mpya “Chibu Perfume” na kuonesha kupokelewa kwa nguvu kubwa nchini
Tanzania, Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kigwangalla ameandika ujumbe kuhusu
perfume hiyo huku akimsifia Diamond kwa kufanya vitu vikubwa pamoja na kukiri
kuwa yeye sio shabiki wake isipokuwa anaupenda muziki wake.
“Sikuwahi kuwa mshabiki wa msanii
huyu kijana @diamondplatnumz, kama nilivyosema hapo nyuma kidogo, japokuwa
nimekuwa nikifuatilia na ku-enjoy muziki wake; Ila toka nimeanza kumfuatilia
nimegundua kuwa, this young man is not only a good entertainer, but also a
talented entrepreneur and businessman.
"He does business in music, he
does a business of entertainment. Sasa naona kupitia kipaji chake cha
ujasiriamali, naona ameamua kuwa muwekezaji, an investor! This is incredible.
Keep stepping up your game son, that’s the way to do it! Hakika wewe umetoka
#NjeYaBox, na Mungu akuongoze ubaki huko huko juu, usishuke!
"I wish wasanii wenzako pia
watoke nje ya box kifikra, wafanye biashara kwenye vipaji vyao, wageuze
changamoto kuwa fursa, waache kulalamika, wapige kazi tu! #HapaKaziTu! Kwa
sababu nyie watu mashuhuri mkigeuza crowds zenu kama chanzo cha solo la bidhaa
zenu, kwa hakika mtafanikiwa sana!
"Changamoto kwenu wadogo
zangu…#chibudangote #chibu #diamondplatnumz 💪🏾#MzeeWaField
#Dr_Kigwangalla #HamisiKigwangalla #SiasaNiVitendo #supportingourown
#MadeInTanzania #Tanzanian #ProudlyTanzanian – Hamis Kigwangalla (Naibu Waziri
wa Afya)
No comments