TAMASHA LA DAR BODABODA SUPER STAR UNITY FESTIVAL KUFANYIKA 13 MEI JIJINI DAR
Kampuni
ya JP DECAUX Tanzania kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la IRI linalojihusisha
na masuala ya maendeleo wameandaa tamasha maalum kwa wadau wa sekta ya bodaboda
la Dar bodaboda Super Star Unity Festival ambalo litafanyika rasmi jijini Dar
es salaam tarehe 13 mei mwaka huu.
Akizungumza leo meneja mkuu wa JP Decaux Tanzania
Bw.Shaban Makugaya amesema tamasha hilo
linatarajia kushirikisha watu kati ya 5000 lina lengo la kutoa elimu ya usalama
wa barabarani kwa madereva bodaboda na abiria kwa madhumuni ya kuzingatia
sharia ya usalama barabarani kwa matumizi ya barabarani.
Ameongeza
kuwa mbali na kupata mafunzo hayo pia tamasha litasaidia kudumisha umoja ushirikiano na mshikamano katika jamii
bila kujali tofauti za dini,kabila na jinsia.
Nae
mkurugenzi mtendaji wa DJ decaux Bw. Eliya Richard amesema tamasha hilo lenye
kauli mbiu “sote ni ndugu” linatararajia kumpata mshindi bodaboda supa star
sambamba na michezo mbalimbali itakuwepo.
No comments