Breaking News

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI KONGAMANO LA WATAALAM NA WADAU WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI


Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la wataalam na wadau wa vyombo vya habari nchini wanatarajiwa  kukutana jijini Mwanza  ili kuadhimisha siku ya uhuru wa habari duniani(WPFD) inayotarajiwa kukutana tarehe 2 hadi 3 mwezi mei 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kaimu mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika MISA TAN Bi. Salome Kitomary  amesema kuwa siku hiyo ambayo itakuwa  ni ya umoja wa mataifa kusherehekea kanuni za uhuru wa habari kwa kuwakutanisha wadau kutoka sekta ya habari ili kujadili changamoto na namna ya kuzitatua katika uhuru wa vyombo vya habari.

Amesema WPFD ni jukwaa ambalo linawakutanisha  wadau wa vyombo vya habari kuwezesha msukumo wa kimataifa kutunga sharia  rafiki za vyombo vya habari ambazo zitawezesha uhuru wa habari katika sehemu husika.

Bi.Kitomary amesema kuwa kongamano hilo pia litajadili na kupata ufumbuzi kuhusu kuanzishwa utaratibu wa usalama na ulinzi kwa wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari kwenye mtandao na nje ya mtandao.


Kauli mbiu  ya kongamano hilo ni “ FIKRA  YAKINIFU  NYAKATI ZA CHANGAMOTO,JUKUMU LA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUDUMISHA AMANI USAWA WA JAMII JUMUISHI”.

No comments