Samia Suluhu: Kero Za Muungano Zitatatuliwa Kwa Mazunguzo Ya Pande Mbili
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi
kudumisha na kuuenzi Muungano wa Taganyika na Zanzibar na kuwahakikishia
wananchi wa pande Mbili kuwa kero chache za Muungano ambazo zimebaki
zitamalizwa kwa mazungumzo kama hatua ya kudumisha Muungano huo.
Makamu wa Rais Mhe
Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Mahojiano na
vyombo Mbalimbali vya habari katika kuelekea katika Kilele cha Maadhimisho ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo sherehe za kitaifa mwaka huu kwa mara
ya Kwanza zitafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Makamu wa Rais
amesisitiza kuwa tangu Muungano huo uasisiwe umekuwa na manufaa makubwa kwa
pande zote Mbili kwani jamii zimefahamiani na kushirikiano vizuri katika
shughuli za kiuchumi na za kimaendeleo hasa uimarishaji wa ulinzi na usalama
kwa wananchi wa pande Mbili.
Aidha,Amesema hatua
zinazochukuliwa za kutatua kero za Muungano kwa haraka ni jambo jema na la
msingi kwani linalenga kuhakikisha Muungano ambao umefikisha miaka 53 sasa
unakuwa ni Muungano wa mfano wa kuigwa Duniani.
Kuhusu elimu ya
Muungano wa Vijana, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema upo umuhimu
mkubwa kwa taasisi za Kiserikali za pande Mbili kuweka mikakati mizuri ya
kuelemisha vijana wa sasa kujua umuhimu wa Muungano ili waweze kuuelewa na
kuudumisha.
Amesema kwa sasa
vijana wengi wanafuatilia sana mitandao ya kijamii hivyo ni muhimu kwa taasisi
za kiserikali zinazoshughulia Muungano kuweka utaratibu wa kupeleka ujumbe
mbalimbali kuhusu Muungano kwa jamii hasa vijana kwa ajili ya kuwaelimisha
faida za Muungano.
Makamu wa Rais pia
amehimiza makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wastaafu nchini
waendelee na jitihada zao katika kuelimisha umma ili kuuelewa vizuri Muungano
kwa ajili ya faida ya jamii nzima na ya Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa
Rais
DODOMA.
25-April-2
No comments