RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA SAFU YA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA. PROFESA KITILA MKUMBO KATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 04 Aprili, 2017 amefanya
mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu Wakuu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof.
Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.
Kabla ya Uteuzi huu Prof. Kitila
Alexander Mkumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt.
Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Leonard
Akwilapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi. Maimuna Tarishi amehamishwa
na kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge).
Bi. Maimuna Tarishi anachukua nafasi
iliyoachwa na Mussa Uledi ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Ave
Maria Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
ambako anajaza nafasi iliyoachwa na Dkt. Leonard Akwilapo ambaye ameteuliwa
kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Ave Maria
Semakafu alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS).
Wateule hao wataapishwa kesho tarehe
05 Aprili, 2017 saa 3:00 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
No comments