HUU NDIO MTIZAMO WA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA JUU YA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2016/17, PAMOJA NA KWAMO WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Mkurugenzi
mtendaji wa jukwaa la katiba Bw. Hebron Mwakagenda akifafanua jambo
mapema leo jijini dar es salaam
Na Frank wandiba
Jukwaa la katiba
Tanzania (JUKATA) limebaini utekelezaji duni wa bajeti ya mwaka 2016/2017 hasa
katika miradi ya kimaendeleo ambapo wamebaini kuwa serikali imepanga kutumia
shilingi trilioni 29.5 katika mwaka wa fedha 2016/17.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam mkurugenzi
mtendaji wa Jukwaa la katiba Bw. Hebron Mwakagenda amesema katika bajeti
ya serikali kwa miradi ya maendeleo kwa mwaka unaoelekea mwishoni ilikuwa
trillion 11.8 sawa na asilimia 40 ya bajeti kuu ambapo hadi kufikia mwezi machi
2017 miezi mitatu kabla ya utekelezaji wa bajeti kukamilika serikali
imepeleka shilingi trilioni 3.5 tu ambayo ni sawa na asilimia 34 ya fedha
zilizopangwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo 2016/17.
Mwakagenda amesema
kufuatia mwenendo huo hafifu wa utekelezaji wa bajeti umetoa
taswira ya wazi kuwa serikali inaweza isitekeleze bajeti ya maendeleo kwa
kiwango cha asilimia 50 hadi kufikia mwisho wa mwaka wa bajeti ambao ni mwezi
julai hivyo kupeleka bajeti ya mwaka 2017/18 yenye mwendelezo kama huo
kutotekelezeka hivyo kufanya azma ya Tanzania ya viwanda kushindwa kufikiwa.
Bw. Mwakagenda
ametoa pongezi kwa Prof Palamagamba Aidan Kabudi kwa kuteuliwa kuwa
waziri wa katiba na sheria kwani anao ujuzi wa kutosha pasi shaka yeyote
kuongoza wizara hiyo muhimu na nyeti pamoja na ushiriki wake akiwa kamishna wa
tume ya mabadiliko ya katiba mpya hivyo amepitia uzoefu ambao utasaidia katika
kuelekea mchakato wa katiba mpya ambao haupo bayana.
Aidha JUKATA limepokea
mtizamo chanya kuhusu taarifa kwamba serikali ya awamu ya tano ina mpango wa
kuendelea na mchakato wa kuandika katiba mpya kwa mujibu wa kauli ya waziri wa
sheria na katiba Prof Kabudi aliyoitoa kwa wabunge wa kamati ya bunge ya na
katiba na sheria kwamba serikali inatarajia kuanza marekebisho ya sheria ili
kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.
Ameongeza kuwa
mchakato wa kuipata katiba mpya ulisimama na na zipo changamoto kuu mbili
ambazo ni busara kuzitafutia ufumbuzi kabla ya kuendelea ili kuweza kupata
katiba mpya ambayo ni sheria ya mabadiliko ya katiba namba nane ya
mwaka 2011 (pamoja na marekebisho yake) na sheria ya kura ya maoni ya mwaka
2013.
No comments