MAPYA YAIBUKA SAKATA LA KUVAMIA MKUTANO WA WAANDISHI, MTATIRO CUF HAINA WALINZI WA CHAMA WENYE BASTOLA
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uongozi, The Civic United Front (CUF) Julius Mtatiro amefunguka na
kusema chama cha CUF hakina walinzi wa chama wenye bastola wala hakina walinzi
wanaozunguka mitaani kufanya doria.
Julius
Mtatiro ametoa ufafanuzi huo leo baada ya Mkurugenzi wa Habari CUF Taifa,
ambaye anamuunga mkono Profes Ibrahim Lipumba
ndugu Abdul Kambaya kukiri kuwa ni kweli wao walituma vijana kwenda
kwenye Kata ya Mabibo kufanya doria.
"Siku
ambapo kikao kinafanyika Vinna Hotel, vijana wetu pia walikuwa kwenye doria,
tulipozungumza na vyombo vya habari tulikiri na tunaendelea kukiri hatuna
sababu ya kukataa kwamba tulituma vijana wetu na walikwenda kwenye doria"
alisema Kambaya
Kufuatia
taarifa hiyo ya Kambaya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, The Civic United Front
(CUF) Julius Mtatiro amefunguka na kusema wao kama CUF hawana walinzi wa chama
wenye bastola hivyo amelitaka jeshi la polisi limtumie huyu Kambaya kueleza
kijana aliyekuwa na bastola yuko wapi na walikodishwa kutoka wapi.
"Leo
amekiri kuwa lile Zombi lililopigwa na wananchi, Mabibo, eti lilitumwa na genge
la Mungiki/Lipumba ili kufanya doria kwenye kata ya Mabibo. Yani eti Lipumba
ana jeshi lake linalofanya doria na kupiga watu mitaani. Sasa Polisi wasitafute
mchawi, huyu Abdul Kambaya aeleze lile zombi lililokuwa na bastola liko wapi na
waliikodisha kutoka wapi? Alihoji Mtatiro
Mbali
na hilo Mtatiro alizidi kusisitiza kuwa wao hawana walinzi wa chama
"Halafu,
eti huyo msemaji wa Lipumba anasema "Zombi" hilo lililokamatwa ni
"mlinzi wa chama". Napenda ifahamike kuwa CUF haina walinzi wa chama
wenye bastola, na pia hakuna chama cha siasa chenye walinzi wanaozunguka
mitaani kufanya doria, wameajiriwa na serikali ipi? Alihoji Mtatiro
No comments