Breaking News

JOKATE RASMI UVCCM, KAIMU KATIBU MKUU UVCCM SHAKA AMESEMA AMEKIDHI VIGEZO VYOTE.


Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) leo umefanya mkutano na waandishi wa habari lengo likiwa ni kujadili mustakabadhi wa nchi yetu na mambo mbalimbali yanayohusu umoja huo.

kaimu katibu mkuu wa uvccm taifa shakha hamdu shaka amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kutatua changamoto zinazoukabili muungano hili kuweza kudumisha muungano,

Pia shaka wamepongeza wananchi wa pande zote mbili ikiwemo Tanzania bara na Tanzania Visiwani kwa kuendelea kuenzi muungano huo tangu hapo mwaka 1964 mpaka hivi sasa.

“Ikiwa kuna mataifa mengi yalijaribu kuungana lakini muungano wao haukuweza kudumu na  kwetu sisi ni jambo la kujivunia kuweza kutimiza  miaka 53 ya muungano.”

Alisema pia wametoa wito kwa vijana wa Dodoma na maeneo ya karibu  kuondoa tofauti ya vyama na usiasa na kujitolea kuungana kushiriki katika maadhimisho hayo ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya taifa letu kuweza kufanya maadhimisho  katika mji wa Dodoma. 

Aidha shaka aliongeza kuwa Inafaamika kuwa UVCCM ni jiko pia ni tanuru linalowapika vijana kuja kuwa warithi wazuri wa serikali na kisiasa. Kufuatia hili UVCCM imefanya mabadiliko katika baadhi ya nafasi mbalimbali kutokana wahusika kuteuliwa kuwa makatibu wakuu CCM wa wilaya hivyo kuacha baadhi ya nafasi wazi.

Kamati ya utekelezaji UVCCM taifa ilikutana tarehe 18/4/2017 katika kikao chake kilichofanyika upanga Dar es salaam na kuteua wajumbe kama ifuatavyo.

Doris H. Obeid – idara ya uchumi uwezeshaji na fedha
Daniel M. Zenda – Idara ya vyuo na vyuo vikuu
Jokate U. Mwegelo – Idara ya uamasishaji na chipukizi
Mohamedi  A. Abdalah – Idara ya organization, siasa na uhusiano wa kimataifa
Islael sostenes   - Idara ya usalama na maadili

Umoja huo pia umekemea vikali kitendo kinachofanywa na gazeti la Tanzanite kupitia machapisho yake ikiwa la tarehe 10 – 16 lenye kichwa kinachosema “UVCCM isafishwe.


Pamoja ile ya na toleo la tarehe 24 – 30 lenye kichwa ” kashfa nzito UVCCM “  umoja huo wa vijana umemtaka mhariri wa gazeti hilo kuomba radhi ndani ya siku saba kabla hatua stahiki hazijachukulia dhidi ya gazeti hilo kwani kitendo hicho ni kudhalilisha umoja wa Vijana CCM na kuwafanya wananchi wasiwe na imani na umoja huo.

No comments