POLISI DAR WATUMIA SILAHA KUWATAWANYA WAFANYABIASHARA MWENGE

Jeshi la Polisi
limetumia silaha za moto kuwatawanya wafanyabiashara katika eneo la Mwenge,
wilayani Kinondoni leo.
Taharuki iliwakumba
wakazi wa eneo hilo mara baada ya polisi hao kuanza kuwatanya wafanyabiashara
hao waliofunga barabara wakishinikiza magari yaruhusiwe kupaki katika eneo
hilo.
Inaelezwa kuwa
polisi wamezuia watu kupaki magari katika eneo hilo hali iliyosababisha
wafanyabiashara hao kutofungua biashara zao leo.
Mmoja wa
wafanyabiashara na shuhuda wa tukio hilo, Musa Godwin alisema polisi walifika
sokoni hapo saa12 asubuhi na kutawanya wafanyabiashara waliofunga barabara
kuzuia polisi magari yasiegeshwe eneo hilo.
"Walifika hapa sokoni saa 12
asubuhi na baadhi ya watu walifunga njia ikasababisha polisi wapige risasi
hewani, hadi sasa wanazunguka hapa kuzuia magari ambao ni wanunuaji wetu," alisema Godwin.
No comments