ASKOFU GWAJIMA AKARIBISHWA KUENDESHA HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI TANZANIA
Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekaribishwa kuwa anaweza
kuendesha huduma ya usafiri wa treni na kutaka wadau wengine wenye nia kama
hiyo wajitokeze.
Katika
ibada iliyofanyika juzi, Askofu Gwajima aliwaambia waumini wake kuwa
amedhamiria kununua treni ya umeme itakayogharimu Sh11 bilioni, baada ya Rais
John Magufuli kuzindua mradi wa ujenzi wa reli pana (standard gauge)
itakayokuwa na kasi zaidi ya treni ya sasa na uwezo wa kuchukua shehena kubwa.
Ujenzi
wa reli uliozinduliwa na Rais Magufuli Aprili 12, utakamilika ndani ya miezi 30
na awamu ya kwanza itaanzia Dar es Salaam hadi Morogoro, treni yake itakuwa na
kasi ya kilomita 160 kwa saa, ikibeba mabehewa 100.
Msemaji
wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), Catherine Moshi alisema kampuni hiyo imebariki uamuzi huo wa kuwekeza katika
usafiri wa reli, lakini askofu huyo anatakiwa kuomba kibali Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments