MAHAKAMA KUU DAR YATUPILIA MBALI OMBI LA FREEMAN MBOWE
Mahakama
Kuu ya Tanzania leo March 2, 2017, imetoa uamuzi wa pingamizi la Serikali dhidi
ya maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Freeman
Mbowe aliyeiomba Mahakama ilizuie Jeshi la Polisi kumkamata akituhumiwa
kujihusisha na dawa za kulevya.
Mbowe
alifungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar
es Salaam, Mkuu wa Upelelezi kanda maalum na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Jopo
la majaji wakiongozwa na Jaji Sekieti Kihiyo wameutaka upande wa mleta ombi
hilo kufanyia marekebisho ya kifungu kwenye maombi ya Freeman Mbowe kuzuia
kukamatwa na Jeshi la Polisi na kumuweka
ndani wakati kesi ya msingi ikiendelea
Baada
ya uamuzi huo, kiongoz wa jopo la mawakili wa upande wa Freeman Mbowe, Jeneral
Ulimwengu alisema nje ya Mahakama baada ya maamuzi hayo kuwa,
“Ombi
limekataliwa kwa sababu hatukuwa na kifungu
ambacho katika sheria zetu kinafanya kazi katika nchi na maelekezo hayo
ni kwamba kwa sababu tuna ‘import’ sheria zetu kutoka Uingereza. Tutafute
kifungu ambacho kinaweza kusaidia kuendesha mashtaka, hiyo kazi itafanyika kati
ya leo au kesho kwa sababu kesi ya msingi bado ipo na itasikilizwa March 8.”
alisema Jenerali Ulimwengu.
Naye
Mweneyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe baada ya maaamuzi hayo ya Mahakama
alisema jopo la mawakili litahamia mjini Arusha kwenye kesi inayomkabili Mbunge
wa Arusha mjini (CHADEMA) Godbless Lema.
No comments