VIWANDA VIWILI VYAPIGWA KUFULI JIJINI DAR KATIKA OPERESHENI TOKOMEZA VIROBA
Afisa
kutoka shirika la viwango tanzania (Tbs) bw Baraka Mbajije akifunga kiwanda cha
Asia organisation limited kilichopo vingunguti sido jijini dar es salaam katika
oparasheni tokomeza pombe aina ya viroba mapema leo jijini dar es salaam
pembeni yake ni afisa kutoka mamlaka ya dawa na chakula (TFDA) bw Kasela
Kasubi.
Afisa
kutoka mamlaka ya ihifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) bw Rogath Enock
akifunga kiwanda cha Global Beverage Company, katikati afisa kutoka shirika la
viwango Tanzania (TBS) bw Baraka Mbajije, kulia kwake ni afisa kutoka mamlaka
ya dawa na chakula (TFDA) bw Kasela Kasubi katika oparasheni tokomeza pombe
aina ya viroba mapema leo jijini dar es salaam
Maofisa
ambao wanashiriki katika oparasheni ya tokomeza viroba wakifanya Ukaguzi katika
moja ya magala makubwa ya kusambazia pombe maeneo ya tabata sigara mapema leo jijini dar es salaam
Afisa kutoka mamlaka ya dawa na chakula (TFDA) bw
Kasela Kasubi akikagua moja vinywaji wakati wa oparesheni tokomeza viroba tabata sigara mapema leo jijini dar es salaam
Moja
ya pombe inayozaliswa na kiwanda cha Aksa organic Production limited cha jijini dar
es slaam
Moja
ya pombe inayozaliswa na kiwanda cha Global Beverage Company
Na Frank wandiba
Mamlaka
ya chakula na dawa (TFDA) imevifungia viwanda viwili vya kutengeneza pombe kali
ya viroba baada ya kubaini kasoro mbalimbali na kubaini ikiemo vifungishio ambavyo
vimekwisha tumika kutumika tena kufungashia vinywaji hivyo vinavyotengenezwa.
Akizungumza
na waandishi wa Habari wakati wa oparasheni ya kutokimeza vinywaji hivyo ambavyo
serikali imevipiga marufuku kuzalishwa nchini mapema leo jijini dar es salaam Afisa
wa chakula na dawa TFDA Bw Kaseya Kasubi amevitaja viwanda vilivyofungwa kuwa
ni Aksa organic Production limited kilichopo vingunguti sido pamoja na Kiwanda cha Global
Beverage Company.
Kiwanda
cha Asia organisation limited kilichopo vingunguti sido ambacho kiliwahi
kufungiwa na TFDA November 2016 kwa kutokuwa na vigezo na kukitaka kiwanda
hicho kuharibu biashara hiyo kwa gharama Yao leo kimekutwa kikiendela na
shughuli kama kawaida.
Alisema
sambamba na kukuta Kiwanda hicho kinaendelea kutengeneza vinywaji hivyo pia
wamefanikiwa kukamata vifungishio vya viroba ambavyo vinaendelea kutengenezwa na
kukamata sunchsti 9272 ya viroba na vifungishio vilivyokwisha tumika ambavyo
vinatumika tena kwaajiri ya kufungashia tena vinywaji hivyo.
Kwa
upande wa kiwanda cha Global Beverage Company ambacho kilibainika kufanya kazi
ya kutengeneza vinywaji usiku na kufipakia katika vifungishio ambavyo vinavyookatwa
baada ya kutumika na kisha kufunga tena.
Aidha
oparasheni hiyo pia imebaini kuwepo na baadhi ya wafanyabiashara kuendesha
biashara zao bila kuwana vibari na wengine kukutwa vibali vyao vilishakwisha
mda wake, kuwepo na wazalishaji ambao wamekuwa wakitumia stika feki katika
bidhaa wanazozalisha kitendo ambacho kinyume na sharia na kinachangia
kuikosesha mapato serikali.
"leo
ni siku ya pili tangu kuanza kwa oparesheni hii kufatia agizo la waziri mkuu
alilolitoa kuwa kufikia tarehe moja mwezi huu kinywaji hicho kisizalishwe
nchini lakini baadhi ya viwanda vinaendelea kutengeneza na kuuza viroba sasa
tumeamua kuwafungia na hatua zingine za kisheria zitachukuliwa "alisema Kasubi.
Naye
Afisa wa baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) Feada Magesa alisema
mazingira ya viwanda hivyo si salama kwa utengenezaji wa vinywaji.
Alisema
kutokana na mazingira kuwepo kwa mazingira yasiyoridhisha wakati wa uzalishaji
wa kinywaji hicho wote watawachukulia hatua kali za kisheria “Alisema”
No comments