Breaking News

TEACHERS JUNCTION; WALIMU IPENDENI KAZI YENU, NI TAALUMA YENYE FURSA ENDAPO WATAAMUA KUWA WALIMU BORA.

Na Joseph Mwalukasa
Taasisi ya kuongeza thamani ya mwalimu TEACHERS` JUNCTION imewataka walimu  kutojutia kusomea ualimu kwakua endapo  atajilaumu hatoweza kuwa na hamasa ya kufundisha vizuri wanafunzi darasani.

Akizungumza wakati wa semina fupi kwa wanalimu watarajiwa katika chuo cha ualimu Vikindu mkoani pwani,Afisa miradi wa TEACHERS` JUNCTION bwana NJAWA SALUMU amesema   taasisi yao ipo kwa lengo la kumpa thamani mwalimu yoyote nchini hasa kwa kumtafutia eneo analolitaka kufanyia kazi hasa katika shule binafsi endapo atakuwa na vigezo  bila kuzunguka na bahasha mwalimu huyo kutafuta kazi.

Afisa miradi huyo bwana SALUMU ameongeza kuwa  endapo mwalimu atakuwa ameipenda taaluma yake ya ualimu itakuwa rahisi kutafutea kila kona na shule binafsi kwakua na.uwezo mkubwa katika taaluma yake na kufanya kushinda soko huria la ualimu.
Kwa Upande wa mmiliki wa shule ya sekondari ya Mwandege Boys bwana ENOCK MRISHA amewaeleza walimu hao watarajiwa kuwa waajiri wengi wanakuwa na wasiwasi sana walimu wazuri kuibiwa ,hivyo amefananisha na wale walimu wenye uwezo mdogo kuhofia kufukuza kazi muda wote hivyo amewataka kujianda vyema kushindana na soko huria.

Hata hivyo taasisi inayoongeza thamani kwa walimu TEACHERS` JUNCTION kwa kushirikiana na wamiliki wa shule binafsi wametoa wito kwa walimu wote kupenda taaluma yao na TEACHERS` JUNCTION itawasaidia kufanya kazi na shule binafsi hapa nchini.

No comments