SAKATA LA TCU KUTAJA KUWEPO WANAFUNZI VILAZA, CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) CHASEMA HAKIJAWAHI DAHILI WANAFUNZI VILAZA
Siku moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) .
UDSM kimeeleza kwamba
hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za
kujiunga na chuo hicho.
Naibu Makamu Mkuu wa
Chuo hicho, Profesa Florens Luoga alisema jana kuwa chuo hicho kimeweka
utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na
sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.
“Sisi hapa ni wakali
kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa
tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya
udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii
tuliyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza:
“Hiki ni chuo,
hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana
tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi tunaowachukua, wote wanakuwa na
sifa stahiki”, alisema
Profesa Luoga alisema uhakiki ambao umefanywa
na TCU na kutoa idadi ya wanafunzi 224 wanaosoma chuoni hapo, kuhakikisha
wanawasilisha ushahidi wa nyaraka zao, wanaufanyia kazi, kwani kuna uwezekano
tume hiyo haina taarifa kuhusu programu zinazoendeshwa na chuo hicho.
Alifafanua kuwa kuna
baadhi ya programu maalumu, ambazo Serikali ya Tanzania imeingia na nchi
nyingine kwa ajili ya kuendesha programu maalum.
Alisema kozi hizo
zimekuwepo chuoni hapo kwa muda wa miaka 40 sasa na zinafanywa kutokana na
makubalino ya Serikali ya Tanzania na nchi husika.
Alisema chuo hicho
kikongwe Tanzania, kutokana na kuwepo makubaliano hayo kimekuwa kinapokea
baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka nje ya nchi na akasisitiza kuwa yawezekana
ndio hao ambao TCU imeshindwa kupata nyaraka zao.
“Yawezekana kuna
taarifa ambazo hazijakaa sawa, tumepokea taarifa ya TCU sisi kama chuo ni
jukumu letu kuitekeleza,” alieleza Profesa Luoga.
No comments