DC SHINYANGA; ATOA MBINU KWA WANAWAKE KUJINASUA NA MFUMO DUME
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika hafla hiyo
Mkurugenzi
wa shirika la Rafiki Geradi Ngong’a
akizungumza
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga akikabidhi baiskeli kwa wawezeshaji
Baiskeli
za msaada zilizokabidhiwa zikiwa eneo la tukio
Mwezeshaji
akijaribu kuendesha baiskeli
Matiro
amesema matatizo ya manyanyaso kwa wanawake kutoka kwa waume zao husabishwa na wao
wenyewe kutokana na kutojishughulisha na biashara mbalimbali na kubaki kuwa
tegemezi kwa mme wake na hivyo kuishi kama mtumwa.
“Ili
kuondokana na tatizo la mfumo dume ndani ya jamii ni lazima wanawake
wajishughulishe na biashara mbalimbali ambazo zitaondoa dhana ya utegemezi,kama
mitaji ipo mnatakiwa mjiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ndipo serikali
itoe pesa kwenu zile asilimia tano”,amesema Matiro
Aidha
amelipongeza shirika hilo la Rafiki kwa kuendelea kushirikiana na serikali
katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hususani kwenye suala
la kumtetea mwanamke na kumuinua kiuchumi, huku akitoa wito kwa wanufaika na
mradi huo kuyatumia mafunzo hayo vizuri ili kuondokana na hali ya umaskini.
Naye
mkurugenzi wa shirika hilo, Geradi Ngong’a amesema mradi huo wa kumwezesha
kijana wa kike kiuchumi, ulianza mwaka 2015 na kutarajiwa kuisha 2018 ambapo
mpaka sasa wameshaunda vikundi vya ujasiriamali 180 kutoka katika kata 15 za
manispaa ya Shinyanga sawa na vijana 3,833 .
Hata
hivyo Ngong’a amesema, mradi huo unahusisha vijana wa kike ambao wapo nje ya
shule kuanzia miaka 15-24 wakiwemo waliobebeshwa mimba,kuolewa ndoa za utotoni,
kuishi maisha magumu kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali pamoja na kuwaunga
kwenye vikundi vya vikoba ili wajikwamue kiuchumi.
Kwa
upande wake mmoja wa waathirika wa mimba hizo za utotoni Christina Charles
ambaye alipata ujauzito mwaka jana mara baada ya kuhitimu elimu ya darasa la
saba ,amesema kabla ya kujiunga na shirika hilo alikuwa na maisha magumu,
lakini sasa ana uwezo kwa kujihudumia mwenyewe kwa kuuza mboga mboga.
Nao
baadhi ya wawezeshaji waliopewa baiskeli hizo Rose Noel na Getruda Ishengoma
wamesema baiskeli hizo zitawasaidia kutembelea vikundi hivyo vya ujasiriamali
kwa urahisi pamoja na kushauri vijana wengine wa kike kujiunga na shirika hilo
ili wapate kujikomboa na umaskini.
Na
Marco Maduhu-Malunde1 blog
No comments