Breaking News

MHE MAKAMBA ASISITISHA KESHO NDIO SIKU YA MWISHO WA KUUZWA WA VIROBA NCHINI

Serikali imesema azma ya kusitisha uingizaji, uzalishaji, wa vifungashio vya vya  pombe  kali maarufu kama (viroba) kuanzia kesho tanzania bara lipo Pale pale.

Akizungumza  na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam  waziri wa mazingira, muungano mhe Januari Makamba alisema  katazo hilo lipo kwa mujibu wa ibara  ya 8 (1) na 14 ya sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake  zilizofanywa kupitia kifungu cha 230(2)(f) cha sheria hiyo.

Alisema zoezi la kusitishwa matumizi ya vifungashio hivyo vya pastiki utaendana sambamba na operesheni maalum itakayoanza kuanzia tarehe 2 ambayo itahusisha kamati za ulinzi na usalama katika ngazi ya wilaya ,mkoa ,tarafa ,kata vijiji pamoja na mitaa.

Mh. Makamba aliongeza kuwa operesheni hiyo watakagua viwanda vyote nchini vinavyojihusisha na uzalishaji wa vileo na vifungashio vya vya kufungia pombe kali kama vimekidhi viwango.

Alisema kupitia Kamati hizi zitawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya opresheni hiyo na kuwasilisha katika ofisi za serikali za mitaa na kisha kuwasilisha nakala ya utekelezaji katika ofisi ya makamu  wa Mazingira.

Aidha  waziri makamba alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wazalisha wakidai zoezi hilo limekuja ghafla, Serikali  ilitoa taarifa  bungeni tangu tarehe 31 mei 2016 juu ya zoezi hilo hivyo kusema  zoezi hilo litafanyika kama lilivyopangwa.

No comments