WAZIRI MKUU MAJALIWA AWATA WAKUU WA MASHIRIKA YA UMMA KUONGEZA UBUNIFU ILI KUONGEZA UFANISI KATIKA MASHIRIKA YAO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mapema leo 28 Februari 2017, ameongoza
mkutano wa siku moja wa watendaji wakuu na wenyeviti wa bodi za mashirika ya
umma, unaojadili nafasi za mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa
Pili ya Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21), Unaofanyika Ikulu
Jijini Dar e Salaam.
Mkutano
huo ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa
Hazina,Waziri Majaliwa amewapongeza wakuu hao ambapo amewataka kuhakikisha
wanaongeza juhudi na maarifa katika mashirika yao ili kusonga mbele.
Akisoma
hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakuu hao
kuongeza ubunifu zaidi ili kuongeza maarifa katika mashirika yao hii ni pamoja
na kujiendesha kwa faida ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kujiendesha.
Majaliwa
amelipongeza Shirika la Nyumba NHC ambalo kwa miaka ya nyuma lilikuwa
likiendeshwa kwa hasara, hata hivyo baada ya kuongeza ubunifu na kuingia kijana
mzawa, wameweza kupiga hatua na sasa wamekuwa wa mfano wa kuigwa huku pia
akipongeza baadhi ya mifuko ya Maendeleo ya Jamii pamoja na mabenki mengine kwa
ikiongozwa na benki kuu, kutokana na kuwa na menejimenti nzuri, ubunifu na
kutumia wataalamu waliobobea katika fani
zao, wameweza kufanya mambo makubwa.
“Kumekuwa
na dhana potofu kwamba Mashirika ya Umma hayatakiwi kufanya biashara, na kwamba yakifanya biashara lazima yapate
hasara inaendelea kubaki kuwa ni dhana potofu. Ipo mifano mbalimbali” ameeleza
Majaliwa huku akitolea mifano ya nchi zilizofanikiwa kwa mashirika ya Umma kufanya vizuri mfano
Mashirika
kama Petrobras la Brazil, Statoil la Norway, CNOOC la China ambayo ni makubwa
na yameweza kuwekeza nje ya mipaka ya
nchi zao.
Majaliwa
amesema mpaka sasa Serikali imeweza kuwa na Mashirika ya umma 264 ambapo kati
ya Mashirika hayo, Mashirika 65 ni Mashirika ya Kibiashara, Mashirika 187 ni
mashirika ya huduma wakati mashirika 12
ni udhibiti. Kati ya Mashirika 65 ya kibiashara, Mashirika 8 yanaendeshwa kwa
ruzuku ya Serikali, wakati Mashirika 57 hayategemei ruzuku ya Serikali.
Awali
akifungua mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph
Semboja amesema malengo ya mkutano ni kukusanya maoni ya viongozi kuhusu nafasi
ya mashirika ya umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa
wa Miaka Mitano, kuzungumzia changamoto tarajiwa katika utekelezaji wa majukumu
haya na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
“Mashirika
ya Umma yana nafasi na uwezo mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa
Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 2016/17–2020/21 wenye kaulimbiu ‘Maendeleo
ya Viwanda kwa Mabadiliko ya Kiuchumi na Maendeleo ya Watu’,” amesema Profesa
Semboja.
Profesa
Semboja aliongeza, “Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais John
Magufuli, mkutano huu umewezakutanisha viongozi kutoka serikalini na mashirika
ya umma kwa lengo la kubadilishana maarifa na uzoefu wa jinsi mashirika haya
yatakavyoiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa maendeleo endelevu.”
Mkutano
huo unajadili namna ya kuboresha mifumo ya kiutendaji ndani ya mashirika na
uhusiano miongoni mwa mashirika na taasisi za serikali, kufungamanisha mipango
ya mashirika ya umma na Mpango wa Pili wa Maendeleo, kutathmini kiwango na aina
ya rasilimali zinazohitajika kuwezesha utekelezaji wa mipango na; kufanya
ufuatiliaji na tathmini ya mipango.
Jumla
ya washiriki 100, kutoka wizara,
mashirika ya umma na mamlaka za udhibiti takribani 52 nchini.
No comments