MHE MAJALIWA AMUAGIZA CAG KUCHUNGUZA MAPATO YA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA ATCL
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali(CAG) kuchunguza ukusanyaji mapato ya Shirika la Ndege Tanzania(ATCL)
Ameyasema hayo jana alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini
Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.
“Nitamuagiza
CAG aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia
mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,”alisema Majaliwa.
Alisema kuwa Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo
amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya
Taifa.
Pia aliwataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika
kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia
upotevu wa mapato hayo.
Katika hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala, Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la
mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.
Aidha, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha
wanazingatia ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
No comments