MAKONDA AITWA BUNGENI KUJIELEZA, KUFATIA KUTOA KAULI ZA DHARAU DHIDI YA BUNGE
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja limewaita mbele ya Kamati
yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda, na DC wa Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya kudharau Bunge.
Maamuzi
hayo ni sehemu ya maazimio manne ya
Bunge yaliyopishwa usiku huu dhidi ya viongo wanaoteuliwa na Rais hasa
wakuu wa mikoa na wilaya, ambapo azimio lingine ni kumtaka Waziri wa TAMISEMI
kutoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya kazi kwa mujibu
wa sheria na kutoingilia majukumu yasiyo yao.
Hatua
hiyo inafuatia hoja iliyotolewa bungeni hapo na Mbunge wa Ukonga, Mwita
Waitara, kufuatia kauli inayodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda inayodaiwa kuwa ni
dharau kwa Bunge.
Pia
Mwita amedai kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wkuu wa wilaya
wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao,
na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda
na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.
Baada
ya hoja yake kukubaliwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mh Andrew Chenge, wabunge
wameijadili ambapo wabunge kadhaa akiwemo Ester Bulaya, Zitto Kabwe, Saed
Kubenea na Joseph Musukuma wamepata fursa ya kuchangia ambapo kwa kiasi kikubwa
wote wameoneshwa kukerwa na kauli hiyo
inayodaiwa kutolewa na Paul Makonda, pamoja na utaratibu wa wabunge kukamatwa
bila utaratibu.
Wakati
mbunge Zitto Kabwe akipendekeza kuitwa mbele ya kamati viongozi waliotuhumiwa,
Ester Bulaya amepasua jipu kwa kusoma ujumbe wa vitisho aliodai umetoka kwa
kiongozi mmoja aliyeteuliwa na Rais.
Akichangia
mjadala huo, Waziri anayehusika na Bunge pamoja na sera Mh. Jenista Mhagama
amewataka wabunge kutomuhusisha Rais Magufuli na makosa yanayofanywa na
viongozi aliowateua ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria Rais ana majukumu
yake, na wakuu wa mikoa na wilaya wana wajibu wao, hivyo kama kuna RC au DC
anakwenda kinyume na sheria au kuingilia Bunge, anapaswa kuwajibishwa mwenye.
Baada
ya mjadala huo, Chenge amewahoji wabunge wanaokubaliana na mapendekezo ya mtoa
hoja, ambapo wabunge wote wameitikia kuunga mkono mapendekezo hayo manne na
kuwa maazimio rasmi ya Bunge.
No comments