KAULI YA MHE MAKONDA AJIBU TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA WEMA SEPETU KUHUSU MASOGANGE
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda ametupa jiwe gizani kwa kumjibu Wema
Sepetu baada ya siku chache zilizopita kuenea kwa sauti yake mitandaoni akiwa
mahabusu huku akimlalamikia mkuu huyo wa mkoa kushindwa kulitaja jina la Agness
Masogange kwenye orodha ya kwanza ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya.
Akijibu
swali kutoka kwa mwandishi wa habari Jumatano hii ofisini kwake wakati akitaja
orodha ya pili ya watuhumiwa wa madawa hayo, Makonda amesema, “Ukitaja jina
kwanza utakuwa unaingia kama vile unajitahidi kuhama.”
“Hebu
wewe kama una taarifa za mitandao sahihi tuambie tu, ndio maana nimesema
tunapokea kwa wenyeviti wa mitaa, tunapokea wapi, wewe kama una taarifa sahihi
wewe tuambie tu. Lakini usiibue taarifa kwa sababu wewe una jambo la kujibu
ukaibua taarifa nyingine tena siyo rasmi, tena nimeeleza hapa ukiwa kwenye
mahabusu au popote pale chini ya usimamizi hata simu huruhusiwi kuwa nayo,”
ameongeza.
“Kwahiyo
bado vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kucheki pia utaratibu gani
uliotumika kwa mtu kujirekodi na kuanza kutoa matangazo wakati upo sehemu
sahihi ya kutoa hizo taarifa.”
Majina
65 ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya yametajwa kwenye orodha ya awamu ya pili
yakiwemo majina makubwa nchini Freeman Aikaely Mbowe, Yusuf Manji, Mchungaji
Josephat Gwajima, Iddi Azan na Hussein Pambakali.
No comments