Breaking News

MFUMUKO WA BEI WA MWEZI JANUARI 2017 UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.8

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2017 jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Wanahabari wakiwa kazini

Na Frank wandiba
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Januari mwaka huu umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.0 mwezi Desemba mwaka jana.

Hali hiyo imechangiwa na kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo, alisema kasi hiyo imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba mwaka jana.

"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 mwezi Januari 2017 kutoka 100.71 mwezi January mwaka jana,"alisema Kwesigabo.

Alisema mfumuko huo wa bei umechangiwa na ongezeko la bei za bidha vyakula na vinywaji baridi hadi kufikia ongezeko la asilimia 7.6 mwaka huu, hiyo ni kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa Desemba mwaka jana.

"Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka wa bidhaa za vyakula majumbani na migawani kwa Januari mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 8.2 kutoka asulimia 7.4 Desemba mwaka jana.

Aidha, Kwesigabo alisema bafiliko la Fahirisi za bei kwa bidhaa zisizo za vyakula limepungua hadi asilimia 3.6 januari mwaka huu ikiw ni kutoka asilimia 3.8 katika kipindi cha Desemba mwaka jana.

Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania kwa kipindi cha Januari mwaka huu, alisema uwezo wake umepungua katika kununua bidhaa na huduma.

Alisema uwezo wa sh. 100 Tanzania katika kununua bidhaa na Huduma umefikia hadi sh.94.42 katika kipindi cha Januari mwaka huu ikilinganishwa na sh. 95.20 ilivyokuwa Desemba mwaka jana.

No comments