TASWE KUWAKUTANISHA VIJANA ZAIDI YA 1000 KUTOKA VYUO VIKUU JIJINI DAR
Mwanzilishi
wa Saccos cha Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TASWE) Dkt. Anna Matindi
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Vijana kutoka
Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi,leo Jijini Dar es Salaam. Kushotoni Katibu wa Chama cha Vijana
Wajasiriamali–Taswe Bi. Adelaida Ngowi..
Mwanzilishi
wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TASWE) Dkt.
Anna Matindi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa
Vijana kutoka Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi,leo Jijini Dar es
Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu wa
Chama cha Vijana Wajasiriamali – Taswe Bi. Adelaida Ngowi, Mwanachama wa Taswe
Bi. Grace Kimaro.
Mwanachama
wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TASWE) Bibi.
Leah Paul Dennis akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, Kutoka kushoto ni Katibu
wa Chama cha Vijana Wajasiriamali–Taswe Bi. Adelaida Ngowi, Mwanzilishi wa
Chama hicho Bibi. Anna Matinde na Bi. Grace Kimaro. Mkutano huo unatarijiwa
kufanyika tarehe 24 Machi, 2017 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Osterbey
huku kauli mbiu yake ikiwani “Badilisha Mtazamo wa Vijana
wajielekeze katika Sekta Binafsi.
Na Frank Wandiba
VIJANA
zaidi ya 1000 kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi kukutanishwa
jijini Dar es Salaam katika kongamano la Kimataifa litakalofanyika tarehe 24
Machi 2017 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa, Osterbay Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam. Mwanzilishi na
mwenyetiki wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania
(TASWE) Bi Anna Matinde alisema TASWE kwa kushirikina na Kikundi cha Kwayaya
Remnant Generation wameandaa kongamano hilo maalum lengo la kuwajengea uwezo na kuwabadilisha
fikra ili waweze kutambua fursa zilizopo katika Sekta binafsi nchini.
Alisema
vijana hao watapewa mbinu mbalimbali za kijitambua na kutambua fulsa zilizopo
hili waweze kuzichangamkia hususani katika sekta binafsi mara watakapo hitimu
masomo yao hivyo kuwaondolea dhana ilijengekwa kwa wengi wao pindi wamalizapo
masomo yako kutegemea ajira kutoka serikalini.
Nae
Katibu wa Vijana Wajasiriamali kutoka TASWE bi Adelaida alisema kongamano hilo pamoja
na kuwakutanisha vijana kwa lengo la kuwapa elimu na ujuzi utakao wasaidia kuwabadilisha
kitazamo ;imejikita pia katika kuwapa uelewa wa namna watakapo maliza masomo
yao ya elimu ya juu wafikirie kujikita katika Sekta binafsi badala ya kutegemea
kuajiriwa.
Aidha
bi Adelaida. Aliongeza kuwa sambamba na kubadilisha mitazamo yao kongamano hilo
litawasaidia kuwaondolea msongo wa mawazo utokanao na ukosefu wa ajira kutokana
na wahitimu hao wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka wakati nafasi ya ajira zikikua kwa kasi ndogo.
Kauli
mbiu ya kongamano hilo ni “Badilisha Mtazamo wa Vijana wajielekeze katika Sekta
Binafsi”.
No comments