ASKOFU GWAJIMA: ASIMULIA MKASA MZIMA BAADA YA KUKAMATWA POLISI
Baada
ya jana Februari 11,2017 Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima
kuachiwa na Polisi baada ya mahojiano yaliyodumu toka Alhamisi kituo cha Polisi
kati Dar es salaam kufuatia sakata la dawa za kulevya, leo February 12 2017
akiwa kwenye Ibada kanisani kwake amesimulia.
"Nilienda
moja kwa moja kwa Kamanda Sirro, nikamkuta na Manji, wakasema wewe na Manji
tunakwenda kuwapima kwa mkemia mkuu wa Serikali, wale watu waliokuwa wanapima
walikuwa wanapima kwa uwazi kabisa, wakapima vitu vyote majibu hamna chochote.
“Waliposema
twende tukapime nilikuwa tayari, na mimi nilisema ndani yangu hata ukiona Pombe
andika umeona dawa za kulevya, nikasema mimi sina tatizo twendeni nyumbani
kwangu na mkikuta hata sigara andikeni ni dawa za kulevya, wakasachi na
hawakukuta kitu”
Tazama
video hapa chini akizungumza
No comments