MKUTANO WA 6 WA BUNGE KUANZA LEO, WABUNGE 4 KULA KIAPO, MASWALI 125 KUULIZWA.
Mkutano wa Sita wa
Bunge unatarajiwa kuanza siku ya Jumanne tarehe 31 Januari 2017 na kumalizika
tarehe 10 Februari 2017 Mjini Dodoma.
Mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki. Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-
Mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki. Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-
1.0 KIAPO
CHA UAMINIFU
Kufuatia uteuzi wa wabunge watatu
walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli hivi karibuni na Uchaguzi
Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017,
kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:-
(i) Mhe.
Alhaji Abdallah Majula Bulembo
(ii) Mhe.
Prof. Palamagamba John Kabudi
(iii) Mhe.
Anne Kilango Malecela
(iv) Mhe.
Ali Juma Ali - (Jimbo la Dimani)
2.0 MASWALI
Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya
kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa
Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa
papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za
Alhamisi.
3.0 KAULI ZA
MAWAZIRI
Aidha, katika Mkutano huu wa Bunge Kauli
mbili za Mawaziri zitawasilishwa kama ifuatavyo:-
(i) Kauli
ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari,
2017.
(ii) Kauli
ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe
31 Januari, 2017.
4.0 MISWADA YA
SHERIA
Katika Mkutano wa
Tano wa Bunge uliomalizika mwezi Novemba, 2016 Miswada mitatu (3) ya Sheria
ilisomwa kwa mara ya Kwanza Bungeni na kupelekwa kwenye Kamati
husika ili ifanyiwe kazi.
Hivyo katika
Mkutano huu wa Sita Miswada hiyo inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni kwa mara ya
Pili, kujadiliwa na kupitishwa na Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 91. Miswada
hiyo ni:-
i.Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya
Shirikishi wa mwaka, 2016 (The
Medical, Dential and Allied Health Professionals Bill 2016).
ii.Muswada wa Sheria ya
Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).
i.Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka 2016. {The Written Laws (Miscellaneous
Amendments)}, Bill, 2016)
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari,
Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DODOMA
30 Januari, 2017.
No comments