RAIS WA GUINEA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA UMOJA WA AFRIKA (AU)
Rais wa Guinea, Alpha Conde
amechaguliwa leo kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU), uchaguzi
uliofanyika katika vikao vya viongozi wa nchi wanachama vinavyoendelea katika
Makao Makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais Conde anapokea uongozi kwa
Rais wa Chad Idris Deby ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa umoja wa hadi.
Rais wa Chad, Idriss Deby (kushoto)
akikabidhi madaraka kwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, Rais Alpha Conde wa
Guinea (kulia).
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ni
kiongozi asiye na maamuzi (ceremonial head of the Union). Mwenyekiti huyu
huchaguliwa na Marais wa Nchi wanachama wa AU ambaye hushika wadhifa huo
kwa mwaka mmoja tu. Uongozi huu huenda wa zamu katika Kanda tano za bara la
Afrika (Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi, na Afrika ya Kati).
Nafasi hii ilianzishwa mwaka 2002
ambayo Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki ndiye alikuwa mwenyekiti wa
kwanza.
|
No comments