MWANZILISHI MWENZA WA TOVUTI YA JAMIIFORUMS MAXENCE MELO AKAMATWA NA POLISI NA KUWEKWA NDANI
Mwanzilishi
wa tovuti ya JamiiForums, Maxence Melo amekamatwa na Polisi jijini Dar es
Salaam kwa kukataa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.
Taarifa
kutoka kwenye tovuti hiyo zinaeleza kuwa Melo amenyimwa dhamana hivyo
atalazimika kukaa rumande mpaka kesho atakapofikishwa mahakamani.
Jeshi
la Polisi linadai kuwa Melo amekataa kuonyesha ushirikiano kwa Jeshi hilo
ambapo walikuwa wakihitaji majina ya baadhi ya watumiaji wa mtandao huo.
JamiiForums
wameeleza kuwa kiongozi huyo (Maxence) alikataa kutoa taarifa hizo kwa kile
alichoeleza kuwa kufanya hivyo ni uvunjwaji wa Sheria na Haki za wananchi.
No comments