VIJANA WAWILI WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA MTAMBO KATIKA MGODI WA MWADUI SHINYANGA
Wafanyakazi wawili wa mgodi wa Williamson Petra Diamond Ltd uliopo Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu mkoani Mkoani Shinyanga wamefariki dunia kwa kuanguka kisha kuangukiwa na mtambo wakiwa wanarekebisha mtambo.
Waliofariki dunia ni Benjamin Zephania (29) na Alex Mashenene (32) wote wakazi wa Mwadui na ujuzi wao ni mafundi mechanical.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 8.35 mchana ambapo alisema kuwa kuanguka kwao kulisababishwa na kukatika kwa kamba iliyokuwa imeshikilia Boom ambalo lilitolewa kwa ajili ya matengenezo.
“Wafanyakazi hao walipanda juu kwa lengo la kutengeneza mtambo aina ya Liebherr Crane wenye namba za usajili T800 DCD uliokuwa umeharibika ambapo kamba waliyokuwa wakitarajia kuunganisha ilikatika na kuwasababishia vifo”amesema Kamanda Muliro.
No comments