KAMPUNI ZA KOREA KUSINI YAAHIDI KUWEKEZA NCHINI
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa makampuni mbalimbali
kutoka Korea ya Kusini ambao wamekuja Tanzania kuona fursa mbalimbali za
uwekezaji. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini
Dar es salaam Septemba 27, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela,
Angelina Mabula (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
makampuni mbalimbali ya Korea Kusini ambao wapo nchini kuona fursa
mbalimbali za uwekezaji nchini. Picha hiyo ilitanguliwa na mazungumzo
yaliyofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 27.
Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Angelina Mbula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu , Kassim Majaliwa akikabidhiwa jezi yanye maneno Hapa Kazi Tu
iliyotolewa na wawekezaji kutoka Korea ya Kusini waliokuja nchini kuona
fursa mbalimbali za uwekezaji. Awali Waziri Mkuu alizungumza na
wawekezaji hao ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 27, 2016.
Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye
pia ni Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na wawekezaji wa kampuni tisa za nchini
Korea Kusini na kumuahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwekeza
katika sekta ya kilimo, viwanda, maji, miundombinu, elimu, afya na
michezo.
Wawekezaji
hao wanatoka kampuni ya Sima textile, ESM, Jusung Solar Engineering,
Seongnam City FC, Yeong Yang City Korea,Ulsan Vocational Training, Egis
Smart City, MBN
Akizungumza
na wawekezaji hao jana jioni (Jumanne, Septemba 27, 2016) kwa niaba ya
Mhe. Rais Dk. John Magufuli, Waziri Mkuu alisema kwamba Tanzania ni
sehemu salama kwa uwekezaji ikiwa na fursa za uwekezaji kwenye sekta
nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda. Licha ya mazingira mazuri ya
uwekezaji pia aliwahahakishia ulinzi kwenye uwekezaji wao
Waziri
Mkuu alisema Korea ya Kusini inashirikiana vizuri na Tanzania hivyo
wanatarajia mengi kutoka nchini huko kupitia wawekezaji hao.
Wawekezaji
hao tayari wamefanya mazungumzo na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Ilemela jijinii Mwanza na kusaini Hati ya Makubaliano (MoU) kwa ajili
ya miradi minne ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya maji, kiwanda cha
nguo, zana kubwa za kilimo na mafunzo ya ufundi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Msafara huo, Bw. Son Young Soo alisema amefurahishwa
na ziara waliyofanya nchini na wapo tayari kuwekeza nchini.
Naye, Bw.
Jihyun Kim wa kampuni ya Yeong Yang City Korea ambayo inashughulikia
masuala ya kilimo cha mbogamboga alisema watawekeza kwenye kilimo
hususan cha zao la pilipili na watajenga kiwanda kwa ajili ya
usindikaji.
Naye
Mkurugenzi wa Klabu ya Soka ya Seongnam Bw. Suk Hoon Lee alisema klabu
yake ipo tayari kuwekeza katika shule ya michezo kwa vijana ili kuongeza
kasi ya maendeleo ya soka
No comments