Mwenyekiti wa mtandao wa kuzuia ndoa za utotoni Bi Valeria
Msoka akisoma tamko hilo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)akisoma
tamko la mtandao huu.
 |
Mwenyekiti wa mtandao wa kuzuia ndoa za utotoni Bi Valeria
Msoka akisoma tamko hilo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)Kushoto
kwake Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadambi hellen kijo Bisimba
na Bi, Rebeca Gyumi mkurugenzi mtendajiwa tasisi ya wasichana Initiative
Na Frank Wandiba
Mtandao wa
mashirika yanayopinga ndoa za utotoni nchini umeitaka ofisi
ya mwanasheria mkuu wa serikali kuondoa kusudio la kukata rufaa juu ya
kesi ya kupinga ndoa za utotoni iliyotolewa hukumu kuitaka
serikali kuondoa baadhi ya vifungu vya sheria ya ndoa ambavyo vinaruhusu
mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri chini ya miaka 18.
Akisoma
tamko hilo mbele ya waandishi wa habari mwenyekiti wa mtandao huo Bi Valeria
Msoka amesema mtandao huo ushitushwa , kushangazwa na kusikitishwa
na taarifa iliyotolewa na mwanasheria mkuu wa serikali kuwa serikali natarajia
kukata rufaa kufatia hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ambayo iliyokuwa inahoji uhalali
wa kikatiba wa kifungu namba 13 na 17 vya sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
Amesema kufatia
hukumu hiyo ambayo ilielekeza serikali kuanza mchakato wa kubadili vifungu hivyo
ndani ya mwaka mmoja kuanzia kutolewa
kwa hukumu hiyo zipo taarifa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali anafikilia
kukata rufaa kupinga hukumu hiyo mahakamani.
Kufatia uhamuzi huo mtandao unashindwa kuelewa
rufaa hiyo inabebwa kwa misingi gani au serikali ina mpango wa
kuendelea kuwa na vifungu vyahivyo vya kisheria viavyoruhusu watoto wa kike
kuolewa chini ya miaka 18 wakati tayali pia waziri mwenye dhamana ya sheria
alishatoa kauli bungeni kuwa serikali ipo mbioni kupeleka mswada wa sheria
kupinga ndoa za utotoni.
Aidha ameongeza
kuwa kitendo cha Mwanasheria mkuu kukata rufaa kuna ashiria kuwa serikali
INA unaunga mkono ndoa za utotoni jambo ambalo lipo kinyumena mkataba wa
kikanda na kimataifa wa kulinda haki na ustawi wa mtoto wa kike ulio
sainiwa mwaka 1989 kwa upande wake Koshuma mtegeti ambaye ni mwakilishi
wa kulinda utu wa mtoto ameitaja mikoa ya Tabora na Mwanza nimoja ya
mikoa inayo ongoza kwa ndoa za utotoni.
Mapema mwezi
uliopita mahakama mkuu ya Tanzania ilitoa hukumu dhidi ya kesi ya
kupinga vifungu vya sheria vinavyo ruhusu mtoto wa kike
kuolewa akiwa na umri chini ya miaka kumi na nane ilyo funguliwa na
mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Msichana Initiative dhidi ya
mwanasheria mkuu wa Serikali.
|
No comments