Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea mbele ya Viongozi na watumishi wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini(TFDA)
hawapo pichani wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini
Dar es salaam.
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia akimkabidhi nyenzo za kazi
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt. Ben Moses kushoto wakati wa
Uzinduzi wa hiyo leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) Bw. Hiiti Sillo wa pili kushoto
akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya
,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia
wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.
 |
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa
maabara za Mamlaka ya Chakula na Dawa
nchini (TFDA )wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini
Dar es salaam.

Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa katika picha ya pamoja na Bodi
ya Ushauri TFDA wakati wa Uzinduzi wa hiyo leo jijini Dar es salaam.
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali
imetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani
ili kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa nje zipatikane nchini.
Akizungumza
hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na
dawa nchini (TFDA), Waziri wa Afya Waziri wa
Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo kuhakikisha viwanda vya ndani
vinatengeneza dawa hapa nchini na kupiga hatua katika uchumi wa viwanda.
“Serikali
kupitia wizara yangu tumetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu
katika viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa kati kwa kutumia viwanda”.alisema
Mhe. Ummy.
Aidha
Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA kwa kushirikiana na Serikali wanapaswa kuhakikisha
viwanda vya ndani vinatengeneza dawa zenye ubora kwa matumizi ya binadamu ili
kupunguza magonjwa yanayotokana na sumu za kemikali zitokananzo na dawa hizo.
Mhe.
Ummy ameongeza kuwa TFDA inatakiwa ishirikiane na Taasisi ya viwango nchini
(TBS) ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa zisizokizi viwango na ubora
unaopaswa kutumiwa na Watanzania.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili kuwawezesha
watanzania kuepuka kutumia bidhaa zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu .
Mbali
na hayo Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa ikusanye mapato kwa wingi zaidi
ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kupiga hatua kiuchumi ili isaidie
wananchi katika shughuli za maendeleo.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt.Ben Moses amesema kuwa
wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri na watayafanyia kazi kwa
haraka na ufanisi ili kuendana na kasi ya “HAPA KAZI TU”.
“Tumepokea
maagizo ya Mhe. Waziri na nataka kumuhakikishia kwamba tutaendelea na kasi yetu
ili kuifikisha nchi yetu kwenye kilele cha maendeleo na Afya bora” alisisitiza
Dkt. Moses.
| |
No comments