YANGA YASHINDWA KUTAMBA UWANJA WA NYUMBANI,YATOKA SARE YA BAO 1-1 NA MEDEAMA YA NCHINI GHANA
Waamuzi wa Mchezo wa leo kati ya
Yanga ya Tanzania na Medeama ya nchini Ghana, wakiziongoza timu kuingia
uwanjani tayari kwa kuanza kwa mchezo huo wa Kombe la Shirikisho,
uliopigwa kwenye Dimba la Taifa jijini Dar es salaam. Mchezo huo
umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana Bao 1-1. ambapo
Goli la Yanga liliwekwa kimyani na Mshambuliaji Donald Ngoma dakika ya
pili tu ya Mchezo kipindi cha kwanza huku Medeama wakisawazisha dakika
17 baadae kupitia mwa Mshambuliaji wake Benard Danso.
Kikosi cha Medeama.
Kikosi cha Yanga.
Wachezaji wa timu ya Yanga,
wakishangilia ushindi wao pamoja na Washabiki wao, baada ya Mshambuliaji
wake Donald Ngoma kuipatia timu yake goli la kuongoza ikiwa ni dakika
ya pili tu Mchezo dhidi ya Medeama ikiwa ni Mchezo wa Mashindano ya
Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Washabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao.
Kipa wa Yanga, Dennis Munishi “Dida” akiiunyaka mpira kwa umaridadi kabisa.
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Medeama, Samuel Adade.
Mwamuzi wa Mchezo huo, Ibrahim Nour El Din akimzawadia kadi ya njano, beki wa Timu ya Medeama.
Mshambuliaji wa Yanga, Amis
Tambwe akijiandaa kuachia shuti kuelekea langoni mwa Timu ya Medeama,
wakati wa Mtanange wa Kombe la Shirikisho, uliopigwa Uwanja wa Taifa
leo. timu hizo zimetoka sare ya kufungana 1-1.
No comments